» »Unlabelled » Hilary Clinton augua ugonjwa wa homa ya mapafu katika kumbukumbu ya wahanga

Hilary Clinton augua ugonjwa wa homa ya mapafu katika kumbukumbu ya wahanga


Bi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari
Image captionBi Clinton akisaidiwa kuingia katika gari
Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amegundulika kuwa na ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.
Akijerea baada ya kupata nafuu
Image captionAkijerea baada ya kupata nafuu
Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.
Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.
Donald Trump alihudhuria hafla hiyo
Image captionDonald Trump alihudhuria hafla hiyo
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO KARIBU TENA

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles