» »Unlabelled » Asali ''inaweza kukabili maambukizi ya mkojo''

Asali ''inaweza kukabili maambukizi ya mkojo''


Asali hukabiliana na maambukizi ya mkojo
Image captionAsali hukabiliana na maambukizi ya mkojo
Asali na maji inaweza kutumika dhidi ya maambukizi ya mikojo katika wagonjwa waliolazwa hospitalini,watafiti wa Uingereza wamesema.
Wagonjwa huwekewa bomba linalotumika kutoa mikojo iliokwama katika kibofu cha mkojo ama hata kuchunguza kiwango cha mikojo kinachotoka katika mwili wa mwanadamu.
Lakini mabomba hayo mara nyengine yanaweza kusababisha maambukizi.
Wanasayansi katika chuo kikuu cha Southampton wameonyesha katika maabara kwamba asali ilio majimaji huzuia baadhi ya bekteria kutotengeza mapande yalio magumu kuondoa ndani ya plastiki.
Mfuko wa mkojo unaowekewa mgonjwa aliyelazwa hospitalini
Image captionMfuko wa mkojo unaowekewa mgonjwa aliyelazwa hospitalini
Asali husaidia katika kusafisha mabomba hayo na kuyaweka safi wakati ambapo yameshikana na vibofu vya mkojo.
Hatahivyo majaribio mengi yatahitajika ili kubaini iwapo ni salama kutumia kwa binaadamu.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles