POLISI watumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji KIGOMA
Jeshi la Polisi Kigoma, limelazimika kutumia nguvu na mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya wakazi wa mtaa wa katosho na kahabwa kata ya kibirizi katika manispaa ya Kigoma ujiji ,waliokuwa wakiandamana kupinga nyumba zao kuwekwa notisi ya kuhama kupisha ujenzi wa bandari kavu.
Hatua hiyo ilikuja baada ya maafisa wa manispaa kuanza kutoa notisi za kuhama ifikapo mwisho wa mwezi huu kwa zaidi ya kaya elfu moja na mbili ambazo tayari zimekwishalipwa zaidi ya shilingi bilioni 12 kama fidia, hali iliyofanya wananchi wapinge na kuanza maandamano ambapo wameeleza kuwa hawaridhiki na fidia iliyotolewa na mamlaka ya bandari hivyo hawataondoka mpaka pale serikali itakapowafanyia tathmini upya na kuwalipa kulingana na hali ya uchumi wa leo ili waweze kuhamia na kujenga sehemu nyingine tofauti na hali ilivyo sasa ambapo fedha walizopewa hazitoshi ununuzi wa kiwanja na kujenga.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa bandari kigoma yudas sukanyi amesema, kazi ya tathmini nyumba katika eneo la kahabwa ilifanywa na manispaa na wao wamekwishatoa pesa zote kulingana na tathmini iliyofanywa na wataalam wa manispaa na wanachosubiri ni eneo hilo liwe wazi ili kazi ya ujengaji wa bandari ya nchi kavu ianze
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment