» »Unlabelled » Chris Brown akamatwa kwa ‘kumtishia’ mwanamke

Chris Brown akamatwa kwa ‘kumtishia’ mwanamke


Mshirikishe mwenzako
Chris BrownImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionChris Brown aliwahi kupatikana na kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani, Rihanna
Polisi nchini Marekani wamemkamata na kumzuilia mwanamuziki mashuhuri Chris Brown kwa tuhuma za kushambulia mtu kwa silaha hatari.
Polisi waliitwa makazi ya Chris Brown na mwanamke aliyeomba msaada saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Malkia wa urembo, Baylee Curran ameambia gazeti la LA Times, kwamba mwanamuziki huyo alimwelekezea mtutu wa bunduki.
Hata hivyo walizuiwa kuingia na ilibidi wasubiri hadi kupata idhini ya jaji kabla kufanya msako wa kutafuta bunduki katika makaazi hayo.
Mwanamke huyo aliyewaita polisi baadaye aliambia vyombo vya habari kwamba walitofautiana na Brown kuhusu majohari.
Alisema alikuwa ameingia kwa Bw Brown akiwa na rafiki yake na mshirika wa kibiashara na alikuwa akiangalia mkufu wa thamani uliokuwa umevaliwa na mwanamume mmoja pale mwanamuziki huyo alipomkaripia na kumtaka aondoke mara moja akiwa amemwelekezea bunduki.
Alifanikiwa kuondoka makazi hayo bila madhara.
Chris Brown ameandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kujitetea na kuwalaumu polisi kwa kumhangaisha.
Chris Brown na RihannaImage copyrightAFP
Image captionChris Brown na Rihanna walirudiana mwaka 2012 lakini wakatengana tena
Wakili wake alifika kwenye makaazi hayo na kumsihi aandamane na maafisa wa polisi. Mwanamziki huyo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya uvamizi.
Chris Brown amewahi kujipata matatani awali, hususan alipomshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mwanamziki Rihanna hapo Februari 2009.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...