» »Unlabelled » Wachuuzi wapigwa marufuku mjini Kigali


  • 27 Julai 2016

Image captionRwanda imepiga marufuku biashara ya uchuuzi barabarani mjini Kigali.

Rwanda imepiga marufuku biashara ya uchuuzi barabarani mjini Kigali.
Agizo lililotolewa na manispaa ya jiji la Kigali limeanza kutekelezwa ambapo hakuna mtu anayeruhusiwa kuchuuza bidhaa zozote barabarani.
Kulingana na agizo hilo, mfanyibiashara yeyote atakayejihusisha tena na biashara hiyo yaani muuzaji na mnunuzi atatozwa faini ya kiasi cha dolla 15 za Marekani.
Wakuu wa mji wa Kigali wanasema biashara hiyo ni kero kwa biashara halali,kwa usalama na pia usafi wa jiji hilo.
Mjini Kigali katikati kabisa sehemu ambako kawaida biashara hii ya uchuuzi au umachinga bidhaa barabarani imekuwa ikishamiri.

Image captionAgizo lililotolewa na manispaa ya jiji la Kigali limeanza kutekelezwa ambapo hakuna mtu anayeruhusiwa kuchuuza

Awali sehemu hii ungeweza kujipatia bidhaa mbali mbali kama vile nguo ,vifaa vya kutumia nyumbani au vyakula kama matunda,mboga nakadhalika….
lakini sasa haiwezikani,waliokuwa wanajihusisha na biashara hii baadhi wanasimama tu hapa wakiwa wameficha bidhaa zao huku wakichungana na walinda usalama.………
''Wanatukimbiza lakini mimi siwezi kuacha kabisa.''Badala ya kulala njaa na mtoto wangu nitakubali kukimbizwa na hata kufungwa jela kwa sababu mimi sijapewa kiwanja sokoni ili niweze kufanyia biashara sokoni kama wengine.''
''Sina nyumba hapa mjini sina kiwanja,sasa wanataka nifanye nini?''
''Nitaendelea kutembeza bidhaa barabarani wakita waniuwe!wakiniuawa watanizika wenyewe,franga elfu 10 siwezi kuzipata.'' walisema wachuuzi ambao hawakutaka kutajwa majina yao.

Image captionFranca hizo elfu 10 ambazo ni takriban dolla 15 za Marekani,ni faini iliyotangazwa na manispaa ya jiji la Kigali itakayotozwa wanaojihusisha na uchuuzi

Franca hizo elfu 10 ambazo ni takriban dolla 15 za Marekani,ni faini iliyotangazwa na manispaa ya jiji la Kigali itakayotozwa wanaojihusisha na biashara ya kutembeza bidhaa barabarani na hata wateja wao.
Akitangaza uamuzi huo Meya wa mji wa Kigali Monique Mukaruriza ametoa sababu tatu muhimu za kupiga marufuku biashara hiyo ambayo hufanywa na watu hohehahe hasa hasa akinamama.
''Hii biashara ni kero kwa usalama wa barabarani na mji mkuu Kigali kwa ujumla''.
''Tunahitaji usalama wa wapita njia wa magari na hata wa wafanyabiashara wenyewe.

Image captionWachuuzi na wanunuzi watatozwa faini ya dola 15

''Biashara hii ni kero kwa biashara iliyo halali kawa sababu hawa wanaotembeza bidhaa hawalipi kodi hali inayoumiza sana wafanyabiashara walipa kodi.''
''Sababu nyingine ni kwamba hii biashara ni kero sana kwa usafi wa mji wetu wakati tunapopigania kuwa na mji msafi,biashara hii haiwezi kukubalika,'' alisema meya Mukaruriza.
Manispaa ya jiji la Kigali limeshatangaza njia mbadala kwa wachuuzi hawa.

Image captionMeya wa mji huo anasema kuwa wachuuzi wanasababisha uchafu

Ikiwa ni pamoja na kuwahamishia katika masoko yao maalumu ambayo yamekwisha jengwa jijini Kigali na kwa wale ambao watajiunga na masoko hayo manispaa imeahidi kuwaondolea kodi kwa kipindi cha mwaka mzima pamoja na kuwasaidia kupata mkopo wa pesa zisizozidi laki 2 Franca za Rwanda ama dolla mia 300 za Marekani.
Agizo hili limeanza kutekelezwa muda mchache baada ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human rights watch kuilaumu serikali ya Rwanda kwa kuwafunga katika vizuizi visivyo rasmi watu lililotaja kuwa masikini wengi wao wakiwa ni wachuuzi hao.
Shirika hilo lilisema uongozi unanuiya kuwaficha wasionekane hadharani,madai ambayo serikali ilitupilia mbali.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...