» »Unlabelled » Vioo vipya vya simu visivyovunjika kwa urahisi

Vioo vipya vya simu visivyovunjika kwa urahisi

  • 31 Julai 2016

Gorilla GlassImage copyrightCORNING
Image captionTeknolojia ya Gorilla Glass sasa hutumiwa katika 70% ya simu za Samsung na Apple
Ni mara ngapi simu yako imekuponyoka, iwe ulikuwa unapiga selfie, au umesahau ulipoiweka na mara ikaanguka?Hasa kwa simu za kisasa zaidi ziitwazo smartphone aghalabu cha kwanza kuvunjika huwa kioo cha juu yaani ‘smartphone screens’.
Visa vya skrini za kuvunjika au kupata nyufa ndio ukarabati nambari moja katika matatizo ya simu aina ya smartphone wakati zinapowasilishwa kwa mafundi ili kufanyiwa marekebisho.
Sasa, kampuni ya Corning inayoangazia utaalamu kuhusu vioo vya simu inasema imefanikiwa kuunda vioo ambavyo havivunjiki kwa urahisi.
Kampuni ya hiyo imekuwa ikiunda vioo aina ya Gorilla Glass ambavyo hutumiwa katika 70% ya simu nyingi za kisasa zikiwemo Samsung na Apple.
Sasa inasema kwa kutumia aina mpya ya vioo hivyo, ambayo inaitwa Gorilla Glass 5, skrini za simu zinaweza kunusurika kwa asilimia 80% wakati zikianguka hata kutoka kwa urefu wa mita 1.6.
Majaribio ya simu zenye vioo hivyo yaliyofanywa kuwaonesha wanahabari kuthibitisha na baadhi yazo ziliangushwa mara hadi 20 kwenye sakafu ngumu ya maabara hiyo bila kuvunjika.


Nyingi ya simu huanguka kutoka urefu wa kutoka kiunoni au mabega ya mtu, kwani huwa zimewekwa kibetini, mifuko ya suruale ndefu au wa shati au zikiwa zimeshikiliwa.
Watengenezaji wa simu wanasema wataanza kuzinadi simu za Gorilla Screen Glass 5 kwenye miezi michache ijayo.
"Tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na wateja wetu, ambao ni makampuni ya simu na wameonesha kufurahia maendeleo hayo," Meneja mkurugenzi wa kampuni ya Corning John Bayne ameielezea BBC.
Hata hivyo amesema umadhubuti wa bidhaa zinazouzwa unategemea zaidi watengenezaji binafsi wa simu na kuwa kila kifaa pia kinategemea matumizi na matunzo ya mnunuzi na mtumiaji.
Kampuni ya Corning imekuwa ikijihusisha na biashara ya utengenezaji na uuzaji wa bidhaa za vioo tangu 1879, ilipotengeneza glass inayotumika kwenye taa iitwayo Edison lightbulb.
Kufikia mwisho wa 2016, zaidi ya simu 4.5 bilioni zitakuwa zimetengenezwa na kuboreshwa kwa teknolojia hiyo ya Gorilla Glass.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...