VITU VYA
KUZINGATIA
·
Kuficha credential zako mf. Neno au namba ya
siri, habari zako binafsi (personal particulars)
Jambo muhimu kukumbuka wakati wa
kununua vitu online ni kuhakikisha unaficha habari zako za kibenki, kwani kuna
wizi mkubwa kwa kutumia mtandao!, watu wamekuwa pia wanafungua tovuti feki ili
kuwalaghai watu!. Pia jaribu kutafuta habari tofauti tofauti kujua athari za kufanya
manunuzi online
·
Huduma za usafirishaji (shipping
services) na waranti.
Pia ni jambo muhimu kuangalia kama kuna huduma
ya usafirishaji, la sivyo, unaweza nunua vitu na bado ukahitajika kutoa gharama
nyingine kuvileta ulipo!. Unapotaka kununua vitu kwa njia ya mtandao, inakubidi
kuangalia tovuti tofauti tofauti kwa
kuwa zinatofautiana kwenye ubora wa huduma, mfano kampuni moja yaweza
uza kitu (item)
bila ya waranti (warranty), lakina nyingine yaweza uza pamoja ya
kutoa waranti ya bidhaa, yaani product
warranty!
NJIA ZINAZOTUMIKA
Credit card
Njia ya kawaida ya kununua vitu online ni kutumia credit
kadi. Hii ni njia kubwa ya kununua vitu online au vitu dukani, ebooks online au
bidhaa ambazo si rahisi kuzipata maduka ya rejareja . Wakati wa kununua kitu na
credit kadi ni lazima kuhakikisha kwamba tovuti ni salama. Kawaida, tovuti
itakuwa na lock kidogo juu yake pia huwa na kiungio cha https badala ya http!.
PayPal
Njia ya pili ya kawaida kwamba watu kununua vitu online ni
kupitia PayPal.
PayPal ni
moja ya makampuni makubwa yanayotuo huduma ya kununua vitu online. Kama tovuti
ni salama na halali, itatoa njia ya PayPal
kama njia ya kuwasilisha malipo. Kufungua akaunti PayPal
ni bure na rahisi sana. tembelea tovuti hii https://registration.paypal.com/na
unaweza kuanza haraka.
eCheck
Moja ya njia ya kawaida kwamba watu kununua kitu online ni
kupitia eCheck.
ECheck inamuwezesha mteja wake kuchukua fedha na kuangalia salio. Akiba katika
akaunti ya eCheck yaweza
kutumika kufanya manunuzi online. Kama unatumia eCheck,
kuwa na uhakika kwamba tovuti ni salama. Njia hii kuchukua muda mrefu sana kwa
mchakato kuliko kadi za credit,
na unaweza kusubiri kwa muda wa hadi siku saba kwa ajili ya malipo kufanyika.
Umuhimu:
Kununua huduma na
bidhaa online ni njia kubwa ya kuokoa fedha
na muda. Ni njia ambayo waweza nunua bidhaa kama za kielektroniki, vitabu na
bidhaa za urembo!.
Angalizo:
Njia hii ya kufanya manunuzi online yafaa kutumika kwa
tahadhari kubwa!, hakikisha unaona kiungio cha https://,
badala ya http//,
pia kiwe na alama ya kofuli kwenye address bar ,
mfano https://www.buyingstuffs.com, vile vile usitumie njia ya manunuzi
isyotambulika/hakikishwa kimataifa au kitaifa! Hakikisha kampuni unayotaka
kununua vitu inatambulika na pia soma masharti na vigezo (terms and
conditions) ili ujue kama uko salama kufanya nao biashara!
Umekaa
nyumbani unataka kununua bidhaa zako lakini hujisikii kwenda duka
lolote la jirani au ‘supermarket’. Usiwaze, mambo siyo kama zamani tena.
Watu wengi hawajui kuwa kupitia simu yako ya mkononi, tabiti, au
kompyuta yenye mtandao, unaweza kununua bidhaa zako na kuzipata kwa
muda mfupi mlangoni kwako.
Kasi ya ukuaji wa Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (Tehama) imefungua milango ya kununua bidhaa
mtandaoni kwa kuyavuta maduka na kupunguza utegemezi wa kununua bidhaa
kwa kuonana na muuzaji.
Kampuni kadhaa za nje na za
ndani kama Kaymu, Hellofood, Kivuko, Jumuia, ShoppingTz na nyinginezo,
zimeanzisha huduma hiyo ili kutumia fursa adhimu ya biashara katika
jamvi la Tehama.
Biashara hii inafanyikaje?
Katika
soko au duka la mtandaoni, mteja na muuzaji hawakutani ana kwa ana,
bali kupitia mtandao kwa kuunganishwa kupitia tovuti au programu ya simu
(‘app’) ambazo nyingi humilikiwa na kampuni za kijasiriamali.
Tovuti
hizo huwa ni jamvi au meza ambazo wauzaji huweka taarifa zao za kina
kama vile bei na aina ya bidhaa, idadi, kiwango, mwaka wa kutengenezwa
(kwa bidhaa za kuisha muda) na uwezo wake.
Taarifa hizo
huambatana na picha halisi za bidhaa ili kuzuia utata unaoweza kutokea
mteja anapokuta bidhaa aliyonunua na kuletewa siyo ile iliyopo pichani.
Programu ya kompyuta inayofanya kazi kama kikapu hutumika kufanikisha
ununuzi kwa kumjulisha mnunuzi jumla ya bidhaa alizonunua na fedha
anazodaiwa.
Katika tovuti hizo kuna kila aina ya bidhaa
kuanzia nguo, vyakula, magari, vitabu, vifaa vya elektroniki, vipodozi,
vidani, muziki, video na vinginevyo.
Malipo
Malipo
katika biashara hiyo iliyoanzishwa miaka 35 iliyopita na mjasiriamali
Mwingereza Michael Aldrich, yanaweza kufanyika moja kwa moja mtandaoni
au wakati mteja anapopokea bidhaa.
Meneja Mkuu wa
kampuni ya kuuza chakula mtandaoni, Sherrian Abdul anasema wateja
wanaweza kulipia kupitia Tigo Pesa (kwa sasa) au kulipia wakati
wanapokea chakula.
Pia, shoponlinetz kupitia tovuti yao
wamebainisha kuwa wateja wanaweza kufanya malipo yao kupitia kampuni za
malipo za Visa, Visa Electron, Paypal, Mastercard, Airtel Money na Tigo
pesa.
Bidhaa kama muziki na video au programu za
kompyuta unaweza kuzipakua haraka mara tu baada ya kuzilipia, wakati
bidhaa kama nguo na nyinginezo zitakuhitaji usubirie kidogo inatokana na
umbali wa duka lilipo na makazi yako.
Changamoto za usafirishaji bidhaa
Pamoja
na mfumo wa kielektroniki kufanya miamala ya biashara husika mtandaoni
kwa haraka, usafirishaji wa bidhaa hadi kwa wateja umekuwa ukikumbwa na
changamoto kubwa ya ukosefu wa anuani za makazi. “Mara nyingi
tunajitahidi kupata taarifa za msingi alipo mteja jinsi iwezekanavyo,
mara nyingi tunaangalia mwanzo wa mtaa au kituo cha basi.
Ila
tunategemea sana kampuni bora za usafirishaji kukamilisha zoezi hilo
ambazo huwapigia wateja na kuwapelekea wateja bidhaa ndani ya muda
unaotakiwa,” anasema Mkuu wa masoko na uhusiano wa Kampuni ya Kaymu,
Angaza Nkurlu.
Hata hivyo, gharama za usafirishaji
zinatofautiana kutokana umbali na ukubwa unaosafirishwa, kwa Kaymu bei
hizo ni kati ya Sh3,000 hadi 4,000 kwa bidhaa ndogo ndogo na umbali wa
kawaida wakati Hellofood ni kati ya Sh2, 000 hadi Sh3, 000.
Mustakabali wa biashara
Mtaalamu
wa Tehama, Jumanne Mtambalike anasema biashara hiyo inakuwa kwa kasi
huku kampuni za kimataifa kama Kaymu na Jumia zikibisha hodi nchini na
kampuni za kizawa za Kivuko, Online Shopping na Gateway na nyingine nazo
zimeonyesha ushindani mkubwa. “Unajua kati ya mwaka 2011 hadi 201,3
biashara za aina hiyo zilikuwa zinafanyika kupitia mitandao ya kijamii
kama Facebook kwa muuzaji kuweka bidhaa anayouza kwenye ukurasa wake au
wa kundi na kuweka mawasiliano ili wateja wanaohitaji wamtafute.
“Lakini
mwaka huu tumeshuhudia tovuti lukuki maalumu kwa biashara hiyo na kwa
taarifa nilizopatiwa hivi karibuni, mtandao wa Kaymu Tanzania unafanya
biashara na watu zaidi ya 1,000,” anasema.
Licha ya
biashara hiyo kukua kwa kasi nchini, baadhi ya wananchi kama Thabiti
Ibrahimu hana uhakika kwamba ununuaji wa bidhaa mtandaoni una usalama wa
kutosha hususan kwenye malipo.
Matukio ya wizi wa
mtandao kupitia mashine za kutolea fedha au fedha kupitia njia ya simu,
anasema yanazidi kumpa hofu iwapo kweli atapata bidhaa yake ikiwa
salama.
Hata hivyo, Mtambalike anasema ni lazima wengi
wapate hofu kutokana kutomjua mtu anayewauzia, huku akiwatoa wasiwasi
katika upande wa malipo kwa kuwa maduka mengi yanataka ulipe wakati
unapokea bidhaa hivyo unaweza kuikataa iwapo umeletewa usiyoihitaji.
“Kwangu
mimi vikwazo vikubwa ni vitatu: uelewa mdogo wa watu kuhusu biashara za
mitandao, ukosefu wa mfumo ulio imara wa malipo na wenye ulinzi wa
kutosha na usalama wa taarifa za mnunuzi na ukosefu wa mtandao baadhi ya
maeneo ya Tanzania,” anasema mtaalamu huyo.
Kwa
Nkurlu, changamoto zilizopo ni fursa yao kuwekeza zaidi kwa kutoa elimu
kwa wananchi namna ya kununua na kuendelea kupeana utalaamu kati ya
wasafirishaji na watoaji huduma kifedha ili kuboresha zaidi biashara
hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment