» » U F U F U O.

  Faraja ya waliokufa katika Yesu Kristo.

Somo hili litatuambia ukweli juu ya watakatifu wa MUNGU. *maana watu wengi wamefundishwa kuwa watakatifu wa MUNGU watanyakuliwa kwa sili* je, ni kweli jambo hili?? Je, watakatifu wa MUNGU watapotea tu au waliokufa watafufuliwa na walio hai watapaa mbinguni kumlaki YESU ajapo mala ya pili?? Na waovu itakiwaje je, watamwona YESU akishuka mawinguni?? na wao kitatokea nini YESU ajapo?? 🤔🤔

Kwa ufafanuzi zaidi gusa link hii
*https://youtu.be/0xYxD6Gj1jM*

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo." (Yohana 11:25)

"Wafu wako watafufuka, maiti zangu zitafufuka, amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini..."(Isaya 26:19)

"Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamuka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele." (Daniel 12:2)

"Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake." (Ufunuo 20:13)

Mwanadamu, aliyeumbwa kutoka mavumbini, hurudi mavumbini wakati wa kufa.

Mungu akamwambia Adamu:

"...hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi." (Mwanzo 3:19)

Mwanadamu akifa hulala katika mavumbi ya ardhi. Ikiwa kama alikufa katika Bwana, atangojea mpaka atakapofufuliwa tena wakati wa kurudi Kwa Yesu Kristo mara ya pili.

NI NINI KILISABISHA KIFO?

"Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. (Warumi 5:12)

"Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu"
(Warumi 3:23)

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti..." (Warumi 6:23)

ATAKAYEWAFUFUA WALIOKUFA NI NANI?

"Amin, amin, nawaambia, saa inakuja, na saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. (Yohana 5:25)

"Na mapenzi yake aliye nipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho." (Yohana 6:39)

"...ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na Uzima wa milele; Nami nitamfufua siku ya mwisho." (Yohana 6:40)

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo" (Yohana 11:25)

Yesu ndiye atakaye wafufua wafu wote.

NI NANI ALIYE NA FUNGUO ZA MAUTI NA KUZIMU (MAKABURI)

"... na aliyehai, nami nilikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu." (Ufunuo 1:18)
Yesu Ana funguo za mauti.

UFUFUO UTAKUWA KTK MAKUNDI MANGAPI?

"Msisitajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu." (Yohana 5:28,29)

"Nina tumaini kwa Mungu... ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia."
(Matendo 24:15)

1.Kuna ufufuo wa wenye haki unaitwa pia ufufuo wa uzima,

2.Na Kuna ufufuo wa wasio haki unaitwa pia ufufuo wa hukumu.

UFUNUO WA KWANZA.

UFUFUO WA KWANZA UTAKUWA LINI?

"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza."
(1 Wathesalonike 4:16)

WATAKATIFU WATAFUFULIWA KATIKA UFUFUO WA NGAPI?

"Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu."
(Ufunuo 20:6)

Ufufuo wa kwanza unaitwaje?

"...Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki" (Luka 14:14)
"Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima." (Yohana 5:29)

Ufufuo wa kwanza unaitwa ufufuo wa uzima, pia unaitwa ufufuo wa wenye haki.

Watakaokutwa wamempokea Yesu, wakiwa hai, siku ya kuja Yesu, nini kitawapata?

"Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele..."(1 Wathesalonike 4:17)

"Angalieni nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika." 
(1Wakorintho 15:51-53)

Mungu atawaamsha wafu, akiwapa tena pumzi ya uhai, na kuiamuru mifupa ipate kuishi.

"Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka, amkeni kaimbeni ninyi mnaokaa mavumbini..." (Isaya 26:19)

Paulo anaeleza kwamba wenye haki;
"Watamlaki Bwana hewani" hawatabakia katika dunia hii. (1Wathesalonike 4:17)

Yesu alisema: "...Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu. (Yohana 14:3,4)

Baada ya watakatifu kufufuka, nini kitatokea?

"Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pande nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu." (Mathayo 24: 31)

UFUFUO WA PILI (WA WENYE DHAMBI) UTAKUWA LINI?

"Hao wafu waliosalia hawakuwa hai hata itimie ile miaka elfu." (Ufunuo 20:5)

Kwa kuwa waovu hawataweza kwenda mbinguni kwa sababu hawakumpokea Yesu kama mwokozi wao, hawana sababu ya kufufuka Yesu atakaporudi duniani. Watabakia katika makaburi yao mpaka miaka elfu imalizike. Ndipo watafufuliwa ili wapate hukumu yao.

Mwishoni mwa miaka elfu, waovu watafufuliwa Kwa kusudi gani?

"Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake." (Mathayo 25:41)

"Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto."
(Ufunuo 20:15)
Watu wa namna gani watakaochomwa moto wa milele?

"Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, Sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. (Ufunuo 21: 8)

Je! Baada ya kuchomwa moto, watenda dhambi watakumbukwa tena?

"Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi." (Malaki 4:3)

"...nao watakuwa kama kwamba hawakuwa kamwe." (Obadia 16)

"Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo." (Zaburi 37:10)

W I T O:

Mwamini Bwana Yesu, ili akufufuwe katika ufufuo wa zima, siku ya mwisho.

"...kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho"
(Yohana 6:40)

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...