» » CCM yatangaza maandamano Aprili 2018

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, wanakusudia kufanya maandamano ya amani Aprili 26, mwaka huu, kuunga mkono na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Maandamano hayo yanakuja ikiwa ni jitihada za kuzima kile walichokiita uhuni unaofanywa na wapinzani wao kisiasa wa kutaka kuharibu amani kwa kuhamasisha maandamano ya kuchochea vurugu siku hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Paschal Mwangwala wakati wa kikao maalumu cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa kazi za Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula kwa miaka miwili uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wajumbe 608 kati ya 748 kutoka kata 19 za jimbo hilo.

Mangwala alisema wana-CCM hawawezi kukaa kimya na kushangilia vitendo vinavyofanywa na wapinzani vya kutaka kuvunja amani, bali wazuie kwa kuandaa maandamano hayo yatakayoeleza kuwa chama pekee nchini ni CCM.

“Saidieni watu waone chama ni CCM peke yake na si vingine vinavyodandia ajenda ya kupiga kelele hiyo Aprili 26, na sisi tusaidiane maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli. Haiwezekani watu waongee vitu vya kipuuzi na kukaa kimya.”

“CCM Mwanza hatuwezi kuvumilia yeyote atakayevunja amani, yeyote atakayeleta chokochoko kwenye mkoa wetu atakiona cha mtema kuni. Yanayofanywa na viongozi wetu wa juu yashuke mpaka kule chini, wananchi waone, viongozi wa mitaa waunge juhudi hizi,” alisema.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela, Nelson Mesha alisema kinachofanywa na vyama vya upinzani nchini ni dalili tosha kuwa vimefikia mwisho na vimekosa hoja na badala yake vinakimbilia kufanya maandamano.

•Tuma Habari, video na picha za matukio mbalimbali WhatsApp au Telegram kwa 0625966236




Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...