» » Waziri Mkuchika Atoa Maagizo Mazito Kwa Waajiri Serikalini

Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amewaagiza waajiri wote wa serikali kuhakikisha wanatoa vielelezo vinavyotakiwa vya watumishi wao ndani ya siku 14 pale wanapoagizwa kufanya hivyo na Tume ya Utumishi wa Umma, kinyume cha hapo watawajibishwa.

Mkuchika alitoa agizo hilo jana alipotembelea Tume hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa. 

Aliwataka waajiri hao kuzingatia sheria kwa kuwa imeelezwa kuwa wamekuwa ndio chanzo cha kuchelewesha kesi za waajiriwa kwa kutokutoa ushirikiano kwa haraka.

“Waajiri zingatieni sheria, pale tume inapotaka kupata vielelezo inataka ijiridhishe. Kesi zinachukua muda mrefu kama hakuna vielelezo lazima zichelewe,” alisema Mkuchika. 

Kwa upande mwingine, aliwataka wafanyakazi wa tume hiyo kutekeleza majukumu yao ya kazi, huku wakijiepusha na rushwa kwa kuwa eneo wanalofanyia kazi lina ushawishi mkubwa.

Pia aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili tume hiyo zikiwemo za rasilimali fedha, watu na usafiri. 

Naye Kaimu Naibu Katibu wa Tume hiyo, Richard Odongo alisema tume hiyo inapokea na kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma ambao hawajaridhika na mamlaka zao za nidhamu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...