» » Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yahadharisha Uwepo wa Mvua Kubwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka wachimbaji wa madini katika migodi midogo midogo kuwa makini kwani ongezeko la maji katika udongo linaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi na maporomoko migodini katika kipindi hiki cha mvua za msimu.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utabiri wa mvua za msimu wa Novemba mwaka huu hadi Aprili mwakani.

Pia imezitaka mamlaka za miji pamoja na wananchi, kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha mifumo na njia za kupitisha maji zinafanya kazi katika kiwango cha kutosha ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu pamoja na upotevu wa maisha na mali.

Akizungumzia mwelekeo wa mvua za msimu, Dk Kijazi alisema kutakuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi yanayopata msimu moja wa mvua kwa mwaka, na kwamba mvua kubwa inatarajiwa Januari mwakani.

“Msimu huu ni mahususi katika maeneo ya magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu Kusini Magharibi, kusini mwa nchi, maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na Ukanda wa Pwani ya Kusini.

Mvua inatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya Novemba na kuisha wiki ya nne ya Aprili, 2018,” alieleza Dk Kijazi. Alisema Kanda ya Kati kwenye mikoa ya Singida na Dodoma, mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya Desemba mwaka huu, zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.

Kwa Nyanda za Juu Kusini Magharibi na maeneo ya Kusini mwa nchi, mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya Novemba na wiki ya kwanza ya Desemba. Alisema Pwani ya Kusini kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya nne ya Novemba na wiki ya kwanza ya Desemba.

Dk Kijazi aliwataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ambao ni wakulima, wafugaji, mamlaka za wanyama pori, mamlaka za maji na afya waendelee kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...