» » Polisi Waua Watuhumiwa Waliomjeruhi Meja Jenerali Mstaafu

KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI NA KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA SMG RISASI KUMI NA TISA NA MAGANDA MAWILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 11.10.2017 majira ya saa nne kamili usiku huko maeneo ya Mbezi Mshikamano kwa Mgalula, askari walipata taarifa kutoka kwa FRANCIS MINDE miaka 30, mfanyabiashara ambaye anamiliki duka la vitu mchanganyiko kwamba walifika watu wawili katika duka lake wakitumia pikipiki aina ya Boxer nyeusi ambayo haikusomeka namba na kumuuliza kama kuna huduma ya M-PESA na TIGO-PESA na kuwajibu kuwa hakuna huduma hiyo, aliwatilia mashaka huenda sio watu wazuri hatimaye alitoa taarifa Polisi.

Mara baada ya kupata taarifa hizo askari walikwenda eneo hilo na kuiona pikipiki ikiwa imeegeshwa gizani ikiwa na watu watatu, askari waliwaita watu hao ili kuwahoji lakini watu hao walianza kukimbia huku wakifyatua risasi upande waliopo askari, kuona hivyo askari nao walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wawili, mmoja kati yao alifanikiwa kukimbia na pikipiki waliyokuwa nayo

Aidha eneo la tukio ilikutwa Silaha aina ya SMG yenye namba UC59821998 ikiwa na magazine mbili, magazine moja ikiwa na risasi kumi na tisa (19) na nyingine ikiwa tupu na maganda kumi na tatu (13) ya risasi aina ya SMG.

Katika ufuatiliaji wa tukio hilo ilibainika kuwa mmoja wa majambazi hao waliouwawa ni miongoni mwa watuhumiwa walioshiriki tukio la kuvamiwa kwa Meja Generali mstaafu wa Jeshi la Wananchi VICENT KARIONGO lililotokea mnamo tarehe 11/09/2017 majira ya saa kumi na moja jioni.

Majeruhi wote wawili walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala. Hakuna askari aliyeumia au kujeruhiwa, miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles