» » Polepole Amchana Zitto Kabwe

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Ndg Humphrey Polepole amerusha jiwe gizani kwa Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe kwamba anajua wakati huu anapitia wakati mgumu sana ndani ya chama ndiyo maana anatapatapa katika suala la makubaliano kati ya serikali  na Kampuni ya Uchimbaji madini ya Barrick.

Akifanya mazungumzo ndani ya Ofisi yake na EATV, Polepole amesema kwamba kitendo cha Mbunge huyo kitendo cha Mbunge huyo kwenda kuzungumza kwenye chombo cha habari na kuuhadaa umma kwamba  madini yataendelea kuwa madini ya watu wa nje, yeye hana tatizo naye kwani anafahamu wazi kwamba chama kinaenda kumfia hivyo watu wamuelewe..

"Naomba mumuelewe huyu bwana, anapitia wakati mgumu. Chama kinamfia tumuelewe sana. Watu wote wenye uelewa mpana  walioshiriki katika kukianziasha chama wote wameondoka na wameondoka kwa masikitiko ya kwamba chama kimepoteza dira. Asubiri kuona matokeo ya maendeleo yanayoletwa na serikali.  Mfama maji haishi kutapatapa ni sehemu ya asili ya ubinadamu. Namwambia asubiri kuona maendeleo yatakuja kutokana na makubaliano haya makubwa" Polepole.

Aidha Polepole amesema kwamba Zitto ameshiriki katika kutunga sheria tatu ndani ya Bunge kuhusu madini kisha akaenda ulaya kusema kwamba madini yatazidi kuchukuliwa na wageni ni kuuhadaa umma kwani katika sheria waliyoitunga ilikuwa ni ya kutamka  kwamba madini yaliyopo ardhini ni mali ya watu wa Tanzania.

Ameongeza pia Sheria ya pili Mh. Kabwe aliyoshiriki ni pamoja na ile ya Kuipa Mamlaka Bunge kutazama masuala ya madini vizuri na sheria ya tatu ikiwa ni kuboresha sheria za kodi ikiwa mapato na bima lakini kwa sababu chama kinaenda kumfia hivyo hataweza kuacha kudandia hoja hata kama hazina mashiko.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...