» » Mbowe Amkaribisha Nyalandu CHADEMA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe, amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu.

 Mwenyekiti Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu.

"Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu  kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu" ameandika Mh. Mbowe.

Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM jana  alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.

Milango iko wazi kwako @LazaroNyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu.

— Freeman Mbowe (@freemanmbowetz) October 30, 2017

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...