» » Maseneta wa Marekani wamemtembelea Rais Magufuli

Rais John Magufuli wa Tanzania, amefanya mazungumzo na ujumbe wa maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani.

Taarifa ya Ikulu ya jana Jumatano imesema  maseneta hao ni wajumbe wa kamati ya mazingira inayoshughulikia hifadhi ya taifa, wanyamapori na misitu ya Marekani.

Maseneta hao wamekuwepo nchini Tanzania kwa siku tatu lengo likiwa ni kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson.

Taarifa ya Ikulu imewataja maseneta hao kuwa ni James Inhofe, Mike Enzi, David Perdue, Luther Strange, Tim Scott na John Thune.

Baada ya mazungumzo, kwa nyakati tofauti maseneta James Inhofe na Mike Enzi wamemshukuru Rais Magufuli kwa kukutana nao.

Pia, wamemshukuru kwa kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani kuja kuwekeza nchini.

Maseneta hao wamesema Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo ni fursa muhimu ya kukuza uchumi.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles