» » Lukuvi atoa tamko kampuni za ndani za mipango miji

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali haitatumia kampuni za wataalamu wa mipango miji kutoka nje ya nchi, badala yake itaendelea kuwatumia wa ndani kutokana na uwezo wao.

Lukuvi amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa Bodi ya Usajili ya Wataalamu wa Mipango Miji jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umeshirikisha wajumbe wa bodi hiyo 150 kutoka kampuni za wataalamu wa mipango miji.

Kwa mujibu wa bodi hiyo, imesajili wataalamu 306 na kati yao 16 wamefutiwa vyeti vya usajili kutokana na makosa mbalimbali.

"Tumeona kazi nyingi zimefanywa na wataalamu wetu wa ndani, takriban asilimia 90 ya kazi zote za uandaaji wa mipango kamambe imeandaliwa na wataalamu hawa, kwa hiyo hakuna haja ya kutumia wengine kutoka nje," amesema Lukuvi.

Katika hatua nyingine, amesema urasimu unaotokana na sheria za nchi umekuwa kikwazo katika miradi inayotekelezwa na halmashauri.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...