» » Lema, Nassari, Msigwa Wawasilisha Ushahidi wao TAKUKURU

Wabunge wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai unaonyesha jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa.

Wabunge wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa jana Jumatatu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.

Wabunge hao wamewasili katika ofisi hizo saa 8.39 mchana na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri.

Katika kile ambacho waandishi hawakukifikiria, wabunge hao waliwasili kwa miguu na kuelekea moja kwa moja ndani ambapo waandishi walizuiwa kuingia.

Ushahidi huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha  kueleza jinsi madiwani wao walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles