» » Uhuru Kenyatta Awakataa Maofisa wa Tume ya Uchaguzi (IEBC)

Chama cha Jubilee cha Rais Uhuru Kenyatta kimewakataa maofisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya wa Urais mwezi ujao Oktoba 17.

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maofisa hao, ambao kimesema wanawafahamu kuwa wanapendelea wapinzani.

Siku moja iliyopita Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza maofisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika Oktoba 17  ambapo miongoni mwa maofisa hao ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na msimamizi wa kituo cha Taifa cha kujumlishia matokeo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limesema "Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maofisa hao kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande fulani."

Leo Rais Uhuru amekutana na viongozi wa kidini ikulu ambapo amesema tarehe iliyotangazwa inafaa ili kutovuruga kalenda ya mitihani ya taifa ambayo imepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Mahakama ya Juu nchini Kenya Septemba Mosi ilifuta matokeo ya Urais  kwa kudai ulikuwa na dosari ambapo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8 ambao Rais Kenyatta alitangazwa mshindi.

Katika uchaguzi wa Agosti 8, Kenyatta alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku mpinzani wake Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Hivi karibuni Muungano wa National Super Alliance (NASA), ambao mgombea wake ni Raila Odinga, ulidai mabadiliko makubwa kwenye IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...