MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
Tulipoishia, Tulienda kupima mpaka DNA ikaonekana mimi kweli ni mama yake. Oooh sasa mbona unasema mambo yameharibika mama kwani kuna nini huko? Aliguna kidogo kisha akasema____Songa sasa...... Yani mambo yameharibika kwani baada ya Zabroni kuujua ukweli huo wote ameanza kulipiza kisasi bila kusikiliza la mtu yeyote hivi ninavyoongea tayari kashauwa watu zaidi ya Ishirini wenye uhusiano wa karibu na huyu mzee. Nashindwa nifanye nini mwanangu ila Zabroni kashawehuka. Nikamwambia sawa mama kwani huyo mzee kashauawa? Akajibu hapana yu hai ila kakimbia haijulikani yuko wapi. Nikamwambia sawa basi mimi ngoja niandae kikosi kwaajili ya kuja kusaidia na kuzuaia mauaji.
Baada ya hapo nijajua mambo yamejipa. Moyoni nilifurahi kwani mbinu yangu ya kuwamaliza majambazi ilifanikiwa bila mashaka yoyote. Nilimwambia mama sawa nimekuelewa nikakata simu. Kisha nikatoka na kukusanya ushahidi wangu tayari kuelekea Wizara ya mambo ya ndani kuwezesha wale majambazi kutiwa mbaroni wote. Basi baada ya kufika huko nikawakabidhi ushahidi wotee na kuwaomba waupitie. Baada ya mda ikaonekana ni kweli Zabroni na kundi lake wanahusika. Mbaya zaidi walikuwemo mpaka mawaziri wa wizara kadhaa.
Nilipongezwa sana na kusifiwa sana. Kila mtu aliniona shujaa. Kisha kikaandaliwa kikosi cha kazi kuteketeza kila kitu katika kundi lile na kuwakamata wote wanaohusika kisha wapelekwe mahakamani. Hawa walikuwa ni wanajeshi wa JWTZ walitoka na kuvamia eneo lile kisha baada ya nusu saa walikusanywa majambazi wote na kuwaleta katika ofisi zile za wizara ya ulinzi na usalama. Waliitwa waandishi wa habari na kuja kuchukua baadhi ya mahojiano.
Nakumbuka mawaziri wengi walikuwamo. Swali la kwanza lilielekezwa kwangu na wakaniuliza nimewezaje kumkamata Zabroni Makweka? Ndipo ukawa wakati wa kuweka ukweli wazi! Nikaanza kwa kusema ukweli ni kwamba Zabroni siyo ndugu yangu. Wala yule mama si mama yake Zabroni. Hii ni mbinu niliicheza mimi na daktari aliyetoa majibu ya DNA. Na hii ilikuja baada ya kuona hali imekua ngumu majambazi walikuwa wengi hivyo ilibidi kuwachonganisha wao kwa wao wauwane kisha mimi nimaluze kazi. Ni kweli Yule mzee alikuwa na danguro na pia yule mama aliwahi kuwa na mahusiano na baba yangu. Lakini haikuwa kweli kwamba Zabroni ndiye kaka yangu ila ilinibidi nimtumie yule mama ila kumuaminiaha Zabroni. Naye bila kufikiri alipita humohumo nilimohitaji apite. Allahamdullillah na tumefanikiwa kuwakamata na sasa amani itarejea.
Mimi na Zabroni hatuna mahusiano yoyote. Ni kufanana tuu kulitokea kutokana na uumbaji wa mwenyezi Mungu hivyo simjui wala hanijui. Duniani wawili wawili na hivyo ndivyo mimi na yeye tulikuwa. Nampa pole kwani kaua watu wake bila kujua. Hakika Nimshukuru baba yangu kwa Ushirikiano japo kwa sasa ni kilema ila haijalishi. Pia nimshukuru mama ambaye ametusaidia sana kuwa mama feki wa Zabroni japo hakulijua hilo ila tulifanya vile ili watu wote akiwemo yeye aishi kwa uhuru na amani.
Zaidi namshukuru Peris ambaye alikuwa mke wangu. Pia alikuwa mpelelezi wa hii kesi na kufanikisha haya yote japo kuna wakati tulitengana na kugeukana kisa kazi. Tuliipenda nchi yetu. Hakika amepumzika Mungu aipokee roho yake na ailaze Pema peponi. Mwisho niombe kesi zote ziende mahakamani na kisha mahakama ziamue hukumu ya kila mmoja kutokana na kosa alilolitenda. Nawashukuru wote mliofika hapa. Pia kikosi cha askari wa JWTZ walifanikisha kukamatwa kwa hawa majambazi. Ila kubwa ni kuwa mama yake Zabroni na mengine watajadiliana jela na Makweka na kundi zima. Hayo mengine tunaiachia mahakama ifanye kazi yake.
Furaha yangu ni kuwa nimefanikiwa kumkamata Zabroni. Namshukuru Mungu kwa hilo. Alitumia kufanana kwangu na yeye kunipakazia maovu. Imenibidi na mimi nit umie kufanana tu kumkamata yeye. Hakika mbinu zote zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Nawashukuru na nisamehewe nilipofanya kosa ila nahitaji haki itendeke. Ahsanteni. Basi watu walishangilia sana na mawaziri walinipongeza na kunipa majina mengi ya kishujaa. Basi mimi pia nilifurahi sana.
Shuhuli ile ikasitishwa baada ya masaa kadhaa kisha Zabroni na kundi lake wakapelekwa mahabusu chini ya ulinzi mkali. Siku iliyofuata wakapelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka yao. Na kisha hukumu ikatolewa. Zabroni na wenzake akiwemo Yule mzee na Pia Jarome Singano wlihukumiwa kifungo cha maisha Jela. Pia wengine vibaraka kila mtu alipata hukumu yake kulingana na hakimu alivyoyaona makosa yao. Baada ya hapo walipelekwa jela na maisha huku nyuma yalibaki yakiendelea.
Nilirudi hospitali nikamchukua baba yangu na pia nikauchukua mwili wa Peris na kuomba msaada wa serikali kumzika. Tulimzika Peris moyo uliniuma sana lakini sikuwa na namna imeshatokea. Niliinamia kaburi nikasali na kumshukuru Mungu kwa yote kisha nikamuaga na huo ukawa mwisho kumwona Peris. Inauma sana. Maisha yalisonga huku mimi nikiahidiwa kupelekwa Marekani kwenda kuchukua mafunzo ya kijasusi. Ili hapo nitakaporudi nilitumikie Taifa kwa weredi zaidi. Swali linalonitatiza mpaka leo ni hili. Wale mawaziri waliohusika mbona hajakamatwa wala kuhukumiwa? Kwanini? Haki ipo? Amka mtanzania tuipiganie Haki.
Haki maofisini, Haki shuleni, Haki vyuoni, Haki katika siasa. Haki kila kona Haki katika jinsia. Haki Haki Haki. Naipenda Tanzania Nitakufa nikitetea haki ya mtanzania. Hakika nchi imebarikiwa sana Milima, mito, mabonde, mbuga, ardhi yenye rutuba. Kwanini hatuendelei? Ni kwasababu ya uongozi mbovu wa baadhi ya watu amka Mtanzania. Tuitafute Haki kokote. Hebu tuimbe kwapamoja huu wimbo...
Tanzania Tanzania nchi yenye mali nyingi.
Watu wengi wa ulaya wanaililia sana.
Naipenda Tanzania ni nchi yangu. Nawapenda wote. Inshaallah tuzidi kuitafuta haki mpaka itakapopatikana.
************Mwishoooo**********
Usikose kusoma simulizi inayokujia hivi karibuni
SIMULIZI YA KWELI-NANI ANIFUTE MACHOZI
ITAKUJIA KARIBUNI KWA LOLOTE MCHEKI MWL KWA
0755683295.
No comments:
Post a Comment