Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 54
Tulipoishia, Tuliikaribia gari mara ghafla wakatokea watu na kufyatua risasi ambazo zilimpata Peris kifuani na baba pia kisha______Songa nayo..... Kisha wakaanza kukimbia, nilibaki nimeduwaa Nisijue nini nifanye kwani ilikuwa ni ghafla sana. Nilimwangalia baba alionekana kajeruhiwa kwenye bega na miguuni. Lakini nilipomgeukia Peris niligundua kuwa hali yake ni mbaya zaidi. Nilimwangalia alikuwa akigalagala mithili ya kuku aliyechinjwa. Niliamua moja tuu kwa kuwa nilikuwa pale hospitali ikanibidi nirudi kuomba msaada. Walikuja manesi na kuwachukua kisha wakawaingiza mawodini.
Baada ya mda mrefu kupita daktari akaniita na kuniuliza mahusiano yangu na wagonjwa. Nilimweleza kua Mmoja ni mpenzi wangu na mwingine ni baba yangu. Akasikitika kiasi kisha akasema pole sana mheshimiwa. Nikajibu ahsante kisha nikamwangalia. Akazidi kusema baba tumefanikiwa kumtoa risasi nafikiri anaendelea vizuri tuu. Ila miguu imeharibiwa sana hivyo atakatwa miguu yote. Na atahitaji uangalizi maalumu toka kwa watu wa karibu. Halafu Mpenzi wako huyo pia tumejitahidi kutoa risasi kifuani zote. Na pia tulikuwa na juhudi za dhati za kuokoa maisha yake lakini alilopanga mwenyezi Mungu binadamu huwezi zuia. Nasikitika kusema juhudi zetu zimefeli.
Ilikuwa ni habari ya kushtusha sana. Lakini kwa jinsi nilivyozoea vifo niliona kitu cha kawaida nikajikuta namwambia daktari ok usijali. Vipi baba anaruhusiwa au? Daktari akaniangalia nadhani alikuwa ameshangaa majibu yangu. Alijua nitapaniki. Lakini kumbe mimi kwangu ni kawaida kabsa.
Basi akanijibu hapana baba anahitaji uangalizi maalumu ila maiti ya Mpenzi utaichukua kesho mochwari. Nikamjibu kuna kazi nafanya nikiimaliza hiyo ndo ntakuja kuchukua maiti kwa sasa naomba niondoke. Namba yangu ya simu ni nikamwandikia kwenye kikaratasi kisha nikamwambia kama hali ya baba itakuwa mbaya tuwasiliane. Apewe matibabu mazuri na ulinzi mzuri ili yasitokee mengine huyo mwingine. Mpelekeni mochwari wakati ukifika ntakuja kumtoa.
Baada ya kuongea hivo kisha nikaondoka zangu. Daktari aliniangalia huku ameshika kiuno. Najua alikuwa akinishangaa mi mtu wa namnq gani nisiyejali kufariki kwa mpenzi wangu. Nilitoka na kutokomea. Nilienda kwenye nyumba moja humo nikaanza kupekua ushahidi ule na kugundua mambo mengi sana juu ya lile kundi. Hakika Peris alifanya kazi. Ndio maana alipostahili kuua aliuwa maana si kwa kazi kubwa kama ile. Nilikuwa najiuliza kama mama yake na Zqbroni alipotea mazingira ya kutatanisha basi bado yu hai. Je kama yuko hai yuko wapi?
Swali langu lilikuja kwani baba aliniambia yule mzee alikuwa na dangulo. Hivyo nikajikuta nahisi kitu. Ndipo nikaamua liwalo na liwe navamia lile Dangulo kisha namtafuta mtu niliyeelekezwa kwa sifa zake. Nilitoka mpaka kwenye dangulo lile. Nilipofika walikuwa wanakuja warembo wengi sana wakihoji. Nataka nihudumiwe ipi? Mbele au nyuma au mdomoni au zote kwapamoja? Aliuliza mrembo mmoja. Nilijisikia hasira nikagamani nimpige makofi ila ningekamatwa mapema sana. Nikamsukuma tuu na kuendelea mbele.
Kisha baada ya mda nikapokelewa na kundi la wamama wa makamo. Wakijidharirisha kwa kutafuta ujira. Haa! Iliniuma sana. Ndipo nikaamua kuuliza mwanamke niliyetajiwa jina. Akaja akasema enhee leo unatakaje? Nikamjibu leo nataka tutoke twende nje nitakulipa wewe ukitoa pesa ya bosi. Alionekana kufurahi ndipo nikatoka naye tukasaini kwa walinzi yaani ilikuwa kama namwiba mtoto wa shule. Mpaka kusaini. Baada ya kufika guest house mi sikutaka kupoteza mda nikamwambia mama samahani. Mimi kilichonileta siyo huduma ni kwamba nina matatizo na matatizo yangu wewe pekee ndiye unaweza kunisaidia.
Yule mama alishtuka kiasi kisha akasema. Ndo nini sasa kunileta huku. Nikamjibu na ndio maana nimekuomba samahani. Naomba unisikilize japo kidogo tuu. Akasema haya ongea haraka! Kwanza nipe hela kabla hujaongea. Aliongeza nikampa kiasi cha pesa kisha alionekana kufurahi kidogo. Nikaanza kwa kumuuliza mzee Ng'ahala unamjua? Alishtuka kisha akasema kwnini? Nikamjibu na ndio maana nimekwambia niko hapa kwasababu. Yule ni baba yangu mimi. Ameniambia alizaa na wewe na mtoto huyo alikuwa anaitwa Samweli. Je kuna ukweli wowote juu ya hilo naomba msaada wako tafadhali.
Akaniangalia kisha akajibu ndio kuna ukweli. Sasa hicho ndicho ulichoniitia? Aliuliza. Hapana mama nina mengi zaidi. Je wajua mtoto huyo alipo? Akajibu hapana! Je ukimwona unaweza kumkumbuka? Akajibu mmmh sidhani. Ni miaka mingi imepita kama 25 hivi na mimi nilizaa nikiwa na miaka 19 sasa ukijumlisha nitakua na 44 uzee unaninyemelea. Nikamjibu ok sawa mama Kwahiyo hujui alipo? Akajibu mwanangu najikuta nakuamini nataka kukwambia kuwa safari ya mapito yangu ya maisha mpaka hapa Mungu anajua kwakweli.
Aliinama akafuta machozi kisha akaendelea. Mwanangu dunia ina watu na viatu. Tamaa iliniponza nilitamani hela nikaishia kujidharirisha. Nilijuwa nimeolewa kumbe naenda kufugwa kama mbwa. Kisha nagawa mwili wangu na uchi wangu kwa kumnufaisha mtu mwingine. Inaniuma sana. Pole mama nikadakia. Ahsante enhee sasa we shida yako nini? Nikasema ok mama ni hivi Zabroni Makweka unamfahamu? Akajibu kwa haraka ndio si mtoto wa bosi wangu.
Ndio huyohuyo. Akajibu namfahamu na amenidharirisha mara nyingi sana. Alikuwa wakati mwingine anatumwa na baba yake aje aniingilie kimapenzi kwa madai ananifundisha. Alikuwa akiniingilia mpaka njia ya gaja kubwa. Nilikuwa naumia na moyo wangu. Nilikuwa natamani kufa lakini ndo dunia ilinigeuka. Zabroni pesa za baba yake zilimpa kiburi sana. Mtoto katili na muuaji yule. Kafanya nini? Aliniuliza. Mmmh nilipata kigugumizi kumwambia kuwa Zabroni ndiye Samweli ndugu wa damu na mimi na pia mwanae wa kumzaa.
Nikajikuta naumauma ulimi na kujizuia kwa mda. Kisha nikamwambia mama ya dunia mengi. Pole sana. Ahsante mwanangu yani kwa yaliyonikuta haya ni baadhi tuu nikikusimulia ni mengi sana. Nikamwbia sasa mama mimi nahitaji kukuokoa humu ili urudi kuishi maisha ya kawaida. Aliniangalia kisha akacheka halafu akasema mwanangu sisi tumeshazoea. Huwezi shindana na yule mzee kwani hadi mawaziri baadhi ni wateja wetu. Kwahiyo hata serikali haitakutetea. Nikamwambia kuna mbinu mbalimbali tayari. Lakini nikiwa naendelea kuongea mara___________
____________________________________________________________
____________ _______________________________________Jamani Yuu (,in ladies voice) umekatisha utamuuuu hahahahahahahah
aahaaa tukutane sehemu ya 55.
[
SEHEMU YA 55
Tulipoishia, Huwezi shindana na yule mzee kwani hadi mawaziri baadhi ni wateja wetu. Kwahiyo hata serikali haitakutetea. Nikamwambia kuna mbinu mbalimbali tayari. Lakini nikiwa naendelea kuongea mara____Songa nayo sasa.........Yule mama simu yake ikaita, Alipokea kisha akaitikia akisema sawa nimekuelewa kisha simu ikakatika. Sikutaka kumdadisi alikuwa anaongea na nani kwani angehisi nipo kwaajili ya kumpeleleza. Nikaamua kuendeleza maada yetu ya mazungumzo huku nikitafakari namna nitakavyomwambia yakuwa Zabroni ni mwanae. Na pia ni kaka yangu mimi. Nilimuuliza kwa mara nyingine mama hivi huyo mwanao huna tetesi zozote?
Akajibu kwakweli sina kabisaa. Nikamwambia aaah sawa mama. Pole kwa yaliyokukuta. Ahsante mwanangu. Sasa mama naomba nikwambie haya. Kila kitu chini ya jua kina sababu na mayokeo yake. Hakuna bibinadamu ajuaye kesho yake. Na laiti kama tungeyajua yatakayojiri mda mchache ujao tusingefanya baadhi ya mambo. Laiti kama mioyo ya binadamu ingekuwa iko nje na unaona kile tunawaziana na kuchukuliana basi binadamu wote tungeogopana maana hakuna akuwaziaye mema.
Binadamu tuna mambo mengi mama. Binadamu tuna vioja, binadamu tuna vituko mama, IPO SIKU MAAJABU YATASHANGAA VITUKO VYA BINADAMU hakuna mwema hata mmoja wote tumeisha tunawaziana mabaya tunatendeana mabaya yani dunia imeisha. Basi yule mama akanikatisha kwa kusema mwanangu inaonyesha umeumia sana nahisi kuna makubwa umefanyiwa lakini hukulipwa mema. Unanikumbusha wakati naolewa na huyu mzee nilifanya kila kitu kwaajili yake ili afurahi lakini haikuwa hivyo. Kumfurahisha kote kumbe kazi bure. Ama kweli mfadhili mbuzi siyo binadamu.
Nikadakia nikamwambia mama, hakuna jema utakalofanya binadamu wasiongee wala kukukatisha tamaa HATA UNGETEMBEA JUU YA BAHARI WATASEMA UNATEMBEA KISA HUJUI KUOGELEA. Binadamu hatuna jema mama. Kikubwa ni kuangalia nini unakitaka katika maisha na kuangalia Mungu anataka nini. Neno msamaha ni dogo ila lina maana kubwa. Vyema kusamehe na kusahau. Kuna mambo mengine ni makubwa je utataka kufa kwasababu tuu ya aibu. Ni vipi dhambi ya kuua uko tayari kuhukumiwa? Laaa ni vyema kuyaacha yaliyopita na kuangalia kubwa moja tuu ni wapi tunaelekea.
Sahau kila aliyekukosea iwe kwa makusudi au kwa kutokukusudia. Huwezi jua Mungu alihitaji ujifunze nini katika mapito yako. Kuongea haya yote nataka ujue kuwa kuna mengi huyajui ila leo utayajua. Je wewe wajua yule mzee ana watoto wangapi? Hapana sijui! Alijibu. Pia unajua Samweli alimchukua kwa malengo gani? Hapana sijui! Alijibu tena. Je wajua Samweli sasahivi ni jambazi anayesumbua nchi hii? Haaa! Samweli mwanangu yuko wapi? Kumbe yu hai? Mwanangu yupo? Haijalishi hata angekuwa ameshakuwa shetani bado ni mwanangu. Siwezi kumkataa kwasababu ya mabaya yake. Yuko wapi mwanangu? Aliniuliza.
Mama yangu Samweli yupo tatizo lipo utakuwa tayari kukubaliana na matokeo? Mi niko tayari mwanangu kwa lolote lile liwe baya au zuri tafadhali. Nikamwambia mama Zabroni ndiye Samweli. Mama alishtuka na kuniangalia mara akaanguka chini puu! Nilimwangalia alikuwa kazimia. Ikabidi nimtoe nje apate upepo kidogo na kwa msaada wa watu wengi zaidi. Baada ya mda alizinduka na kuanza kama kushangaa hivi. Nikamwinua na kumrudisha ndani. Kisha nikamweleza ya kuwa hana sababu ya kujuuta kwani chanzo siyo yeye wala chanzo siyo Samweli. Hata Samweli hajui nini kinaendelea.
Allahamdullillah Mama alinielewa kwa uzuri na akatuliza munkali baada ya maongezi ya mda mrefu. Tatizo likaja Zabroni atajuawaje? Nani wa kumwambia yale yote? Je ataamini? Hapo ndipo ikabidi tuanzishe tena maada nyingine ya mazungumzo ya jinsi gani tutawezesha Zabron ajue kuwa Makweka siyo baba yake. Tuliongea kwa mda mrefu na hatimae mama akajitosa kwenda kumw eleza Zabroni ukweli wote. Tulikubaliana na kumwachia jukumu hilo. Kisha nikampa mama hela ya matumizi pindi akirudi mle ndani. Nilimuahidi kuwa siku chache zijazo watakuwa huru. Kwani nilijua baada ya Zabron kuambiwa yale nini kitafuata. Kazi yangu ilikuwa inaisha kiulaini sana kwakweli.
Tuliagana kisha mi nikarudi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani niliamua kwenda kumwona baba yangu hospitalini. Nilifika nikamkuta naye niliongea naye mambo mengi sana. Alkuwa na wasiwasi sana. Ilikuwa ni juu ya usalama wake. Nilimhakikishia kuwa kwa tulipofikia hali siyo mbaya. Chamsingi ni kumwachia Mungu kila jambo. Hakika yeye hututia nguvu pale tunapokata tamaa na kujisahau kuwa sisi ni viumbe wa Mungu.
Siku zilienda na maisha yakasonga huku nikiwa bado sijachukua mwili wa Peris toka mochwari. Nakumbuka vizuri sana ilikuwa siku ya Jumapili ambapo yule mama alinipigia simu. Nilipokea na kuongea naye. Mwanangu huku mambo yameharibika! Nilijitahidi kumwekeza Zabroni kwa kadri tulivyopanga. Tulienda kupima mpaka DNA ikaonekana mimi kweli ni mama yake. Oooh sasabona unasema mambo yameharibika mama kwani kuna nini huko? Aliguna kidogo kisha akasema______________________________________
____________________________________________________________
_______________ Tuombe uzima 56 yaja nawapenda wote na pole kwa kuichelewesha nimezidiwa kidogo na mitihani ya mwisho so nikimaliza kama kawa kama dawa mambo mengi mazuri yanafuata.