» » Serikali yalifungia Gazeti la Mwanahalisi miaka miwili

Serikali imelifungia Gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili. Imesema hatua hiyo imefikiwa kutokana na mfululizo wa matukio ya ukiukwaji wa misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari, kuandika habari za uchochezi na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abassi ametangaza uamuzi huo leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari.

Dk Abassi amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2017.

Amesema kwa muda mrefu idara hiyo imekuwa ikiwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.

Amezitaja baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo ni ile iliyotolewa Januari 5 iliyobebwa na kichwa cha habari "Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM".

Dk Abassi amesema, "Habari hii ilisheheni nia ovu dhidi ya Rais wakati suala husika lilihusu Shirika la Elimu Kibaha, wahariri walikiri udhaifu wakaomba radhi na kupewa onyo kali."

Amesema Gazeti la Mwanahalisi toleo la  jana lilichapisha makala yenye matusi, dhihaka na maneno yasiyofaa dhidi ya Rais John Magufuli.

"Tulipowaita wakajitetea kwa kutumia neno mubashara yaani walichukua maneno yanayotolewa mitandaoni. Serikali imeona utetezi huo ni dhaifu kwa kuwa habari lazima izingatie maadili," amesema.

==>Taarifa kamili ipo hapo chini


Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...