» » Polisi Wataja Chanzo cha nyumba ya Zitto Kabwe Kuwaka Moto

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe juzi jioni.

Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Amesema  joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.

Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.

Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la  Nyembo Mustafa ametaja  thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...