» » Mbunge wa CCM amtembelea Tundu Lissu Nairobi

Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Samuel Nyalandu amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu jijini Nairobi nchini Kenya kumjulia hali kufuatia mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

Lazaro Nyalandu amesema kuwa kwa niaba ya watu wa Singida na Watanzania wote ametoa salamu za pole kwa mke wa Tundu Lissu kwa kuwa bado hajapata nafasi ya kumuona kiongozi huyo na kusema anasubiri kama ataweza kupata nafasi ya kumuona  kama madaktari wataruhusu.

"Nimefika hospitali ya Nairobi mapema leo (jana) kumjulia hali Mh. Tundu Lissu. Madaktari wanaendelea kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona. 

"Kwa niaba ya wana Singida na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku  endapo madaktari wataruhusu" alisema Nyalandu

Aidha Mbunge huyo amewataka Watanzania kijumla kuendelea kumuombe Mbunge Tundu Lissu ili aweze kupona na kurejea nchini akiwa mzima wa afya njema

"Cha muhimu zaidi, sote tuendelee kumuombea Mungu amtendee wema, na kumponya katika majira haya ya kujaribiwa kwake. Katika yote ndani ya yote, ikawe heri kwake" alisema Nyalandu

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma na baadaye kusafirishwa kupelekwa jijini Nairobi Kenye kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko akiendelea kupata matibabu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...