» » Kikwete asikitishwa na uzushi unaozagaa mitandaoni

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na taarifa za uzushi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za kumhusu yeye akionekana kujibu moja ya kauli ya Rais wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli kitu ambacho si kweli.

Kikwete ametumia mtandao wake wa twitter kuonyesha masikitiko yake hayo kwa watu wanaofanya jambo hilo huku akionyesha kusikitishwa zaidi na mapokeo ya watu ambao wengi wao wameamini hiyo kauli wakidhani huenda ni kweli imetoka kwake kitu ambacho si cha kweli

“Nasikitishwa sana na uvumi huu unaosambazwa juu yangu. Inasikitisha sana. Inasikitisha zaidi kuwa wako watu timamu wanaoamini uzushi huu,”ameandika rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye ukurasa wake wa twitter

Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo mstaafu kuzushiwa uzushi na watu kupitia katika mitandao ya kijamii ambapo mara kwa mara amekuwa akiwasihi wanaofanya hivyo kuacha mara moja

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...