» » Hatukatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya Dawa lakini ni Lazima Yawe Mbali na Hospitali

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali haikatazi Watumishi wa Afya kumiliki maduka ya dawa lakini ni vizuri wakazingatia kuweka maduka hayo mbali na Vituo vya Afya vya Serikali na Hospitali ili kusiwe na aina yoyote ya kutanguliza maslahi yao kwanza katika kutoa huduma za dawa kwa wagonjwa.

Ameeleza kuwa kwa sasa Serikali imejitahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na imeamua kuanza kununua dawa kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa awali.

"Watendaji badala ya kuwaandikia wagonjwa dawa zilizo kwenye orodha, wanaandika dawa zao na kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa kwenye maduka ya dawa. 

"Hatukatazi Watumishi kuwa na maduka ya dawa ila muhimu kuchora mstari wa dawa za Serikali na dawa ambazo sio za Serikali.”  Amesema  Waziri Ummy Mwalimu.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...