» » Bulembo Abadili Msimamo Agoma Kugombea tena CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa madai kuwa anaamini kati ya wagombea 48 waliojitokeza wanatosha.

Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi CCM amesema hatogombea tena nafasi hiyo na amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo na kueleza kuwa awali alichukua fomu kutokana na shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.

"Leo nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa Katibu Mkuu wa chama ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo

Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo atakuwa ameshajiondoa mwenyewe. 

Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.

"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi nyingine,  hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea lakini kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini kwa upande wangu sitagombea" amesema. 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...