» » Urusi yatia mguu mgogoro wa Korea Kaskazini, yaitahadharisha Marekani

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov amemwambia waziri wa Ulinzi wa Marekani, Rex Tillerson kuwa kuiwekea vikwazo vingi Korea Kaskazini hakutasaidia chochote kutatua mgogoro uliopo kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje nchini Urusi imesema kuwa viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio yanayofanywa na Korea Kaskazini.

Lavrov amesema kuwa diplomasia ndio njia pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana.

Hata hivyo, Waziri wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini ili iweze kuachana na mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia huku Rais Trump akisema mazungumzo sio suluhisho

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...