MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 49.
Tulipoishia, Aliniangalia kisha akaniuliza we kijana vipi usaidiwe nini na hiyo silaha. Nikamjibu nahigaji kuonana na wa.................... Kabla sijmalizia mlio wa risasi ukasikika puuuhh!!!!!! _______Songa nayo........Nikiwa nashangaa ni wapi mlio umetokea nikamwona yule mlinzi akianguka chini. Nilishangaa nikapepesa macho huku na huko lakini sikuona mtu wala kiashiria chochote cha usalama mdogo. Nikajua tuu hapa kuna namna haiwezekani ikawa hivi kwanini mlinzi apigwe? Nikaanza kusogea mbele huku nikinyatanyata kwa mwendo wa kukwepa shari. Nilinyata mpaka kwenye kordo ya nyumba ile ambapo nikaanza kuingia ndani na hapo ndipi nikahisi ndani kuna watu kama wanatembea vile.
Sikujua wanaelekea wapi ikabidi nitafute mbinu za kuingilia mle ndani. Chaajabu ni kuwa mlango ulikuwa wazi hivyo nilivyousukuma hivi sikupata shida nikanikuta niko ndani. Wale watu sikuwaona na nikawa nashangaa mbona punde nilisikia sauti zao? Nikabaki nimeduwaa mara kwa mbali nimasikia sauti zikiongea nje ya geti. Nikatoka mbio kwenda kuangalia. Nilipofika nikawaona wao ndiyo wanawasha pikipiki na kuondoka taratibu. Nilijaribu kurusha risasi Loo!Salalehkumbe haina risasi. Nilinisikia vibaya sana kwakweli.
Kwa kuwa nikiwa nashangaa shangaa nikasikia mlio wa gari la polisi. Nikajua tayari kesi nauziwa hapo ndiponikaamua kuruka ukuta na kutokomea. Nilinivuta mpaka kwenye ule uzio wenye umeme. Nklijizuia mpaka nikajikuta nimefanikiwa. Ile nilivyofika tuu chini sikutaka kupoteza mda nikaanza kukimbia. Nilikimbia sana mpaka nikafika sehemu nikahisi usalama kiasi na kuamua kutulia hapo kama sehemu ya mqpumziko yangu. Nilikaa hapo kwa mda na hatimaye nikaondoka. Lakini kichwani nikawa najiuliza ni nani aliyempiga mlinzi. Na alimpiga kwa sababu gani? Au alikuwa ananilenga mimi kisha akanikosa?
Lakini baada ya mlinzi kufa si alikuwa na uwezo wa kuniua. Hapana hakuwa na lengo la kuniua huyu. Nikaamua kujipa moyo kwa kusema potelea mbali kama ni mtego walitaka waninase wamenikosa sasa. Na kama kuna malengo yao mengine hawatafanikiwa hata kidogo. Nilifika mafichoni kwangu na kutulia kwa mda. Maisha yakasonga siku kadhaa zikapita bila mimi kutoka nje. Baada ya hapo nikaamua kutoka na kuendelea na kazi yangu. Nakumbuka siku moja nikiwa katika pitapita za mitaa ya kariakoo nikapishana na mtu niliyehisi kama namfahamu. Baada ya kugeuka nimwangalie vizuri alionekana kukwepa hicho kitu na kuamua kukaza mwendo.
Kwakua nilishamtilia shaka sikuona kazi mimi kugeuka na kuanza kumfuatilia. Alipogeuka aliniona kuwa na mimi nimegeuka namfuatilia akaanza kusukuma watu na kuwa kama aliyepagawa. Alikiwa akitaka kukimbia kwa nguvu lakini kwa umati ule wa Kariakoo angewezaje? Mimi nikawa naenda taratibu bila shida. Mpala alifanikiwa kupita kundi kubwa la watu na kuingia ile mitaa ya jirani ya kariakoo. Nilizidi kumfuata lakini hapa nikapunguza kujionyesha kwani kila alipogeuka hakuniona. Nikamwona amefika sehemu anashusha pumzi ndefu kama mtu aliokoka kutoka mdomoni mwa mamba mwenye njaa kali. Alifanya ishara ya msalaba na kisha kujifuta.
Wakati anamalizia kujifuta anainua mikono akakutana na miguu ya mbabe. Yuu alikuwa ameacha njia ya haki kisa serikali kutokujali watu wake. Baadhi ya viongozi waliokuwa madarakani walikiwa hawatendi haki hali oliyofanya baadhi ya wazalendo kubadili njia zao. Alishtuka sana aliponiona nimesimama mbele yake kwani alijua kifuatacho ni kifo na si kitu kingine. Basi hapo akainua kichwa na kuniangalia ndipo sasa kumbukumbu ikanijia vizuri ya kuwa yule ni miongoni mwa wafuasi wa Zabroni ambaye alinisumbua sana siku za nyuma. Kama alivyojitabiria hapakuwa na kitu kingine zaidi ya kuua ili nipunguze majambazi.
Nikatoa kisu changu kikali na kumc homa kichwani maeneo ya utosini bila huruma. Kisha nikavuta kisu changu na kukifuta damu nikakitia kwenye koti langu safari ya kurudi kwangu ikaanza. Huu ulikuwa ni utaratibu nikiuua inabidi mirudi ndani kwani nikizidi kuzurura ipo hatari ya kushikwa kwani tayari nitakuwa nimeweka taharuki miongoni mwa watu.
Nilifika nyumbani nikaa nikitafakari baba yangu huko wapi lakini sikupata majibu. Je ametekwa au kafa? Wapi baba yangu ulipo? Niliumia sana juu ya baba yangu kwakweli. Basi baada ya mda nikaamua kwenda ufukweni walau nikapunge upepo hata kidogo. Nilitoka nyumbani mpaka ufukweni huko nilikaa kwa mda mrefu nikitafakari mwisho wa yale yote yanayojiri. Nilizidiwa na mawazo nikajikuta naiminya glass ya naji niliyokuwa nimeishika mkononi. Baada ya kutuliza kichwa na kujipa moyo ya kuwa kwasasa nimekwisha punguza majambazi wengi sana hivyo siku si nyingi nitamaliza na kumkamata Zabroni pamoja na watu wake wakiwemo vigogo wa Taifa hili kwani nao wamo.
Nikiwa natoka ufukweni nulitembea umbali mrefu sana huku nikitafakari mambo mengi kama ilivyo kawaida kwangu. Nilitembea mpaka hapo nilipopata usafiri na kuamua kutmrudi mafichoni kisha siku ya pili niendelee na kazi yangu. Nilifika pale kwangu nilipokuwa najificha na kukuta hali tofauti. Kwanza nilikuta nje yaani nyuma ya ile nyumba kuna pikipiki aina ya baja iliyokuwa na namba za usajili PT 67_____ Nilishtuka sana kwani nikahisi huenda polisi waneshajua naficho yangu.
Lakini nilipotaka kukimbia nikakumbuka ndani mwangu ndio kila kitu nimeficha humo. Hivyo ikiwa ni polisi na yupo ndani bora kuua kisha nihame maficho. Nikaamua kuelekea ndani. Nilipofika mlangoni nilikuta mlango uko wazi. Niliingia kwa kunyata na huku nikiwa na tahadhari kubwa. Nikapepesa macho chumbani ambako niliona mtu ambaye kwa haraka nilijua tuu ni Peris kwani haikuwa rahisi kuto kumjua ukizingatia alikuwa mfanyakazi mwenzangu kwa mda mrefu. Zaidi alikuwa mke wangu hivyo kumtambua ilikuwa rahisi. Nikaamua kumwangalia vizuri ndipo nikajua kuwa ni kweli yule ni Peris. Basi hasira ikapanda. Nikakumbuka kuwa mateso yale yote ninayopata Peris anahusika nikasema liwalo na liwe ama zangu ama zake. Naingia humo kama nikifa kwaheri na kama nitapona basi Peris kwaheri. Nikaachomoa kisu changu na kisha nikaingia kwa kasi mara ghafla____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Je nini kilijiri? Kutana na mwl Yuu sehemu ya 50 upate majibu ya swli hilo. Kwa lolote mawasiliano yapo juu tuwasiliane. Nawapenda wote.......Chaoooooo
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 49.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment