» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 48.


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
SEHEMU YA 48.
Tulipoishia, Niliweka begi langu mara kile kinachoashiria hatari kilipiga kelele. Nilishtuka sana nisijuwe ni nini. Mara yule askari akaniangalia kisha akasema hebu fungua begi. Kwa woga nikafungua na kukutana na____songa nayo......Pakti fulani zikiwa zimefungwa vizuri sana ili zisionekane ni nini. Mara yule askari akaichukua moja na kuifungua ndipo ikagundulika ni madawa ya kulevya. Aliniiangalia kama aliyekuwa haamini vile kisha akaamuru askari kadhaa wanikamate na kuniingiza chumba cha mahojiano. Nikachukua begi langu huku nikitetemeka tayari kwenda kuhojiwa na makachero wale wa uwanja wa mwalimu Nyerere.
Niliningizwa humo kisha nikaanza kuulizwa wewe ni nani. Nikajieleza mambo mengi sana mpaka nikatoa vitambulisho vyangu vyote mpaka vya kipindi nikiwa askari. Niliawaeleza jinsi nilivyofika pale mpaja nilivyoishi Ethiopia. Lakini chaajabu kuna askari kama wawili hivi walikuwa wako na kiherehere sana. Walifikia hatua ya kuniomba pesa ili niachiwe huru. Niliwaangalia sana kisha nikahisi wale wako mbinu moja na Zabroni na yule mchungaji. Hapo nikaona hakuna njia nyingine ya kupata haki zaidi ya kuanzisha noma mule ndani.
Nilimwangalia mmoja alikuwa kalegeza mikono huku kashika bunduki. Hapo nilipoona hivyo nikajua tayari mchezo kwisha nikajitia kama nainuka huku najinyoosha kisha kwa ghafla nikampiga teke la sehemu za siri yule askari. Hali ile ilimfanya aachie bunduki na kujishika sehemu hiyo. Kabla bunduki haijafika chini niliidaka na kuiweka sawa kisha nikamkaba mmoja kama ngao vile. Kisha kilichofuata ni kumimina risari bila huruma na kuwalaza chali wale maaskari uchwara waomba rushwa. Baada ya kumaliza nikamsukuma yule niliyemshika na kufyatua risasi iliyotua juu ya kichwa na kumfanya apoteze uhai palepale.
Nilichukua kitambaa fulani mle ndani nikajifuta kisha nikajiweka sawa. Nikachukua begi langu na kutoa madawa na kuyaweka pale ndani kisha mi nikafungua mlango na kuanza kuondoka bila wasiwasi. Nilifika nje nikapitiliza moja kwa moja mlango wa kutokea ambapo nilifanikiwa kutoweka bila kushukiwa na yeyote. Nikafika sehemu moja nikaomba yule wa taxi anishushe kwani nilihisi kama watagundua mapema taxi zote zitaanza kukamatwa hivyo ilikuwa ni lazima nitumie akili. Niliposhuka pale nikaanza kukata kona za vichochoro vya jiji la Dar es salaam mpaka nikatokea eneo langu la mafichoni.
Baada ya kufika nilishusha pumzi ndefu kisha nikaingia ndani ambapo dalili zilionyesha baba hayupo. Hii ilinishtua kwani baba nilimwacha pale. Na hapakuonyesha kama kuna purukushani zozote zilitokea kwani vitu vilikuwa viko salama kabisa. Nilizunguka mle ndani nikiangalia kwa makini kila chumba lakini baba yangu sikumpata. Nilijikuta simanzi inaanza upya kwani sikuwa najua baba yangu alipo mpaka mda ule. Nilikaa chini nikafikiria hatimae nikapata wazo nimpigie simu mama ili nimuulize huenda baba karudi kijijini. Ndipo nikaichukua simu yangu na kuiweka line na kisha nikampigia mama.
Baaada ya maongezi kidogo nikamuuliza vipi baba yupo kijijini? Akajibu hapana hayupo na tangu alipotekwa siku ile hakuwahi kumwona zaidi ya mimi kumpa taarifa ya kuwa niko naye nyumbani. Nikamwambia mama kila kitu akabaki analia tuu kama ilivo ada kwake. Basi mimi nikaona huu siyo mda wa kupoteza niwaze namna ya kumpata baba, pia kukamata wale wajinga mmoja baada ya mwingine. Sikutaka ushirikiano na mtu yeyote kwa sasa. Basi nikaamua asubuhi ya siku inayofuata niamke na kuianza kazi yangu rasmi.
Nililala na asubuhi nikaamka na kujipanga tayari kwa kulia mingo maeneo yote hatarishi. Nilitoka nikiwa nimevalia kofia ambayo ilisukiwa rasta. Lengo ilikuwa ni kuto kukamatwa na pia kutokushitukiwa. Niliingia mtaani huku nikimtafuta Zabroni kwa udi na uvumba. Nilijiapiz a kumuua popote nitakapomwona. Niliingia mitaa mbalimbali bila mafanikio. Mara nikiwa katika mtaa mmoja kwa nyuma yangu niliona pikipiki inakuja niliko na kisha yule aliyekuwa kapakiwa nyuma alijaribu kukwapua simu yangu lakini hakufanikiwa. Ndipo nikamwona akitoa bastola na kuanza kunifyatulia risasi ovyo.
Kwakuwa tayari mwendeshaji alikuwa kapoteza mwelekeo. Hali ile iliwafanya wasifanikiwe kunipiga hata risasi moja. Baada ya kuishiwa risasi waliongeza mwendo na kutokomea. Nilijaribu kuifuatilia kwa kukimbilia lakini sikufanikiwa. Nilichoambulia ni namba za pikipiki tuu basi. Nilishajua kuwa wale hawakuwa watu wema hata kidogo kwangu mimi. Nikasomga mbele na hatimaye nikafika sehemu pikipiki ile imepaki nje na kulikuwa na jumba la kifahari kiasi. Kwanza nilihisi ni mtego lakini pia nilikuwa na shaka na ile pikipiki kwani i kama waliifanyia uhalifu wasingeweza kuitelekeza pale na kisha kupelekea wao kukamatwa.
Hali ile ilinifanya nifikirie mara mbili. Na zaidi nikawa nawaza hawa ni akina nani? Je ni vibaka wa kawaida au ni mtandao mmoja na Zabroni Nikaamua liwalo na liwe mimi ni polisi japo nimesimamishwa kazi. Hapa ninaingia na kama nikiwakuta ndani ni halali yangu. Basi nikatoa bastola yangu na kujiweka sawa kisha taratibu nikasogea getini na kugonga geti. Mara nikashtuka bunduki iko mbele ya kichwa changu huku mtu akiwa kakaza sura. Nilimwangalia alionekana ni mlinzi mkatili sana. Aliniangalia kisha akaniuliza we kijana vipi usaidiwe nini na hiyo silaha. Nikamjibu nahigaji kuonana na wa.................... Kabla sijmalizia mlio wa risasi ukasikika puuuhh!!!!!! ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Je nini kilijiri? Risasi ilipigwa wapi? Na kwa nini? Hatma ya afande yuu ni nini? Kama huna majibu ya maswali haya tukutane sehemu ya 49, nikupe majibu. Nawapenda sana watu wangu byeeeeeee. byeeeeeeee

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...