» » SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 47


MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap,instagram@mwalim_yuu, Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala.
.
Tulipoishia, Nilishtuka kumwangalia mara mbili kisha nikamvua lile dubwana na kushitushwa na ninachokiona mbele yangu. Alikuwa ni mtu ambaye sikutegemea kabisa. Oscar, Oscar, Oscar hata wewe. Mpaka unaamua kuwa mke ili unizunguke vizuri?Alikuwa akilia tuh na kisha akanambia_____Songa nayo..... Bro samahani sikuwa na jinsi kisha akatajichoma na kitu mwilini alikuwa kakivaa mkononi. Mara akaanza kulegea taratibu na kisha akapoteza uhai mbele yangu. Nilibaki nimeganda nisijue nifanye nini mpaka wakati ule kwani nilihisi kila mtu ni adui yangu. Mpaka Oscar. Ama kweli mfadhili mbuzi ipo siku utakunywa hata mchuzi. Nilijiinamia pale bila kujua kwa kuelekea. Nilibaki nimeduwaa mle ndani ya ile hoteli mara mlango ukagongwa. Nilikuwa hata sijielewi nikaenda kufungua bila hata kufikiria mara nikahisi kama nawaona polihisi hivi. Nikawekwa chini ya ulinzi kisha nikafungwa pingu na kupelekwa mahabusu ya kituo fulani pale Adis Ababa Ethiopia.
Nikaingizwa humo kwani waliona kabsa kuwa akili yangu imesimama. Wakaniacha kwa mda hicho ndicho nilipenda kutoka kwa polisi wa Ethiopia tofauti na sisi hapa Tanzania ukimkamata mtu hata hujiulizi kwanini kawahivyo ni ngumi mateke, virungu na matusi. Lakini kule baada ya kugundua siko vizuri waliniingiza mahabusu. Baada ya masaa kadhaa wakanitoa na kuanza mahojiano. Niliamua kuwaeleza ukweli juu ya maisha yangu mpaka mimi kufika Ethiopia nimeingia kwasababu ya kumfukuzia Jambazi niliyekuwa nimefanana naye na pale nina nyaraka zote muhimu. Nikatoa vitambulisho vyangu mpaka vya kazi kuonyesha mimi nilikuwa Askari wa Jeshi la polisi.
Walinisikiliza kwa makini na kunionea huruma kama wanausalama wenzangu. Wakasema wao watanisaidia kwa namna moja tuu watanipeleka ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia. Nikasema pia nitashukuru halafu wakasema ile maiti ya Oscar wataisafirisha kuirudisha Tanzania bila ubalozi kujua halafu huku watatoa maelezo ya kuwa yule alikuwa ni muhalifu nchini Ethiopia. Basi walifanya hivyo mpaka kunifikisha mimi ubalozini ambako nilipokelewa vizuri sana.
Nilikaa nyumbani kwa balozi siku kadhaa huku nikimweleza matukio ya nyumbani. Nilimpenda sana kwani alionyesha uzalendo juu ya Tanzania. Akaahidi kunisaidia ambapo akasema kuwa atatafuta watu ambao nitashirikiana nao kumtafuta Zabroni na kumtia nguvuni. Kisha yeye ataandika barua yenye ripoti maalumu kunihusu mimi. Barua hiyo itapelekwa kwa Raisi wa Tanzania na kisha sitasumbuliwa kwani yote niliyoyafanya ni katika harakati za kutetea Taifa langu. Nilimwelewa vizuri sana ila nikaamua kumkatalia ishu ya yeye kutafuta watu eti nishirikiane nao kumkamata Zabroni. Nikamwambia mheshimiwa mimi simwamini mtu yeyote.
Akaniuliza sasa tutafanyaje kazi hii nikamjibu ikiwa nitashindwa pekeayangu basi nitaachia wengine lakini mimi sitaki kuendelea na yeyote. Mengi yametokea kwasababu ya kumwamini mtu. Simwamini mtu yeyote hata atoke mbinguni. Mheshimiwa kama wataka kunisaidia ni wewe kinifanya nifuke tu Tanzania mimi Zabroni nitahakikisha namkamata mwenyewe. Au kama ni kuweka wasaidizi wekeni lakini wawe kivyao na wasijulishwe kuwa mimi nimo ili kama niwasaliti niweze kuwajuwa mapema. Alikubaliana na wazo langu na kunipa mkono wa kila lakheri katika shughuli nzito ya kumkamata Zabroni. Jambazi aliyekuwa kajikamilisha lila idara.
Basi maongezi yetu yaliishia hapo yaliyokuwa yanamuhusu Zabroni. Tukawa tumemaliza kwa namna hiyo. Basi tukaendelea na mipango mingine ya safari ya jinsi ya mimi kuridi Tanzania. Baada ya kukamilisha mipango ambapo ilipaswa niondoke Ethiopia baada ya siku mbili. Siku zilisonga na hatimaye mda wa kurudi Tanzania ukawadia. Mchakato mzima wa safari yangu uliratibiwa na Ofisi za ubalozi. Nilifurahishwa sana ambapo nilipelekwa uwanjani kwa u safiri mzuri na nilifurahia kwakweli. Hapo ndipo nilijua umuhimu wa ubalozi kwa nchi zinazoshirikiana.
Nilifika uwanjani nikachukua ndege na safari ikaiva kurudi Tanzania. Pembeni nilikaa na mtu aliyekuwa amevaa kichungaji alikuwa akisoma biblia mda wote. Lakini kama ujuavyo safari bila soga haiendi. Taratibu alianza kunichokonoa kwa maswali ya kizushi. Nilikuwa namjibu kwa mkato Sana lakini hakukata tamaa mpaka baada ya mda nikajikuta namzoea. Aliniuliza nashukia wapi kati ya Nairobi au Dar es salaam kwani ni kuwa ile ndege haikuwa ikitoka mojq kwa moja Ethiopia mpaka Tanzania. Ika ilikuwa inapitia anga la Nairobi na kutua kisha safari kuendelea kama kawaida.
Baada ya kuwa tumeongea sana mi nikapitiwa na usingizi. Nililala mda mrefu kidogo. Lakini wakati nimelala kulikuwa kama kuna kitu nakiona nikiwa usingizi ule wa mawenge. Hua kuna baadhi ya matukio unayaona ila unashindwa kuyazuia kwakuwa umelala. Basi mimi nilikuwa nahisi kama mtu anafungua begi langu mara kadhaa. Sikua najielewa kwani nilikuwa usingizini japo nacho yalikuwa yakiona kwa mbali. Sikulijali hilo mi nikapiga usingizi sana tuu.
Yule mchungaji alikuwa anakuja mpaka Tanzania. Baada ya kufika nairobi yule mchungaji alishuka na kupotea. Sikujua hata alipoelekea lakini mizigo yake ilibaki kwenye ndege. Baadhi ya mabegi yake yalikuwa pale kwenye kiti alichokuwa amekaa. Basi mimi nikajua atarudi tuu. Mpaka ndege inaacha Ardhi ya Kenya alikuwa hajarudi. Sikulijali hilo kwani mimi nilikuwa naangalia nafasi yangu kama mimi. Baada ya kufika Dar es salaamu tulishuka na kuanza kukaguliwa. Niliweka begi langu mara kile kinachoashiria hatari kilipiga kelele. Nilishtuka sana nisijuwe ni nini. Mara yule askari akaniangalia kisha akasema hebu fungua begi. Kwa woga nikafungua na kukutana na___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Je aliona nini? Mwalimu yuu ana majibu kaa karibu na mm nikupe uhondo. Nawapenda woteeee. Samahani kwa kutoipata simulizi kwa wakati majukumu yamezidi. 48 iko njiani byeeeee.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...