» » Saida Karoli Adai Kutishiwa Kuuawa......Aahirisha Show zake Kujinusuru

Ikiwa imepita miezi miwili toka msanii wa nyimbo za asili Tanzania Said Karoli arudi rasmi kwenye muziki na kuachia kazi zake mbili zilizopata mafanikio na kuwafikia watu wengi zaidi ameibuka na kudai watu wameanza kumpiga vita kishirikina na wanataka kumuua

Said Karoli ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Orugambo' amedai kuwa ushirikina upo na watu wanampiga vita ili aweze kupotea tena kwenye muziki kama ilivyotokea kipindi cha nyuma na kudai kuna mtu amelipwa pesa ili amuuwe kabisa jambo lililopelekea kuahirisha baadhi ya show zake.

"Huyo mtu alinielekeza watu kadhaa ambao wamepanga mpango wa kuniua aliniambia, sasa mimi nimeshalipwa nikuuwe nikuondoe duniani kabisa yaani kabla ya kufika Mwanza, Geita tena bora hata hizi show zingine uvunje, kweli ramani aliyonipa nilichoka ikabidi show zingine za Bukoba tumezivunja tukasema ngoja tutulie kwanza tuone nini kitaendelea" alisema Said Karoli

Saida Karoli anakiri wazi kuwa suala la ushirikiana lipo na kwake si jambo la ajabu kumtokea kwani tayari ameshakutana na mambo ya namna hiyo sana na kudai yeye anamtegemea Mungu na kumuomba Mungu.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles