» » Prof. Mkumbo Ammwagia Sifa Raila Odinga.....Adai ni baba wa Demokrasia Afrika

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amepongeza hatua zilizochukuliwa na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga za kwenda mahakamani kudai haki yake.

Amesema kuwa kipindi ambacho kina Odinga wanapambana kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi, Uhuru Kenyatta yeye alikuwa kivulini

Prof. Mkumba amesema kuwa Raila Odinga ni mwanasiasa aliyekomaa kidemokrasia hivyo anafaa kuitwa baba wa demokrasia barani Afrika huku akiwataka wanasiasa kuiga mfano huo.

“Ahsante sana Raila Odinga kwa hakika maamuzi uliyofanya kwenda mahakamani kutafuta haki ni maamuzi sahihi, wewe ni baba wa Demokrasia katika ukanda huu,”amesema Prof. Mkumba.

"Huyu Kenyatta ni beneficiary. Wakati akina RAO wakipambana na akina Moi yeye alikuwa kivulini. Tuwe wa kweli" amesisitiza Kitila Mkumbo 

Uchaguzi mkuu nchini Kenya umefanyika hivi karibuni ambapo mgombea kutoka chama tawala cha Jubilee, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na kumbwaga Raila Odinga 

==>Chek apo chini
 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles