» » Mtatiro: Bora CCM kuliko kufanyakazi na Prof. Lipumba

Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amejibu baadhi ya hoja za watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya Serikali kumtambua.

Amesema kuwa hilo ni jambo ambalo halitawezekana tena kwao kukubali yaishe, hivyo hawawezi kukaa meza moja na Profesa Ibrahim Lipumba kwani alishaga jiuzuru katika harakati za Kampeni za uchaguzi.

"Nasoma maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali, dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali yaishe? Lipumba apewe kila kitu...hadi roho zetu, lakini misingi yetu, misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile anazozitizama msaliti" alisema Mtatiro   na kuongeza;

"Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba"

Aidha Mtatiro amesema kuwa ni rahisi sana kufanyakazi na Chama cha Mapinduzi CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Ibrahim Lipumba kwakuwa alichokifanya si kitendo cha kiungwana.
 
Julius Mtatiro kwa sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo na ayasema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe. 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...