» » Polisi Watoa Majibu ya Uchunguzi Ofisi za Mawakili wa IMMMA Kulipuliwa Bomu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.

Walinzi hao wanadaiwa kukutwa baadaye maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.

Imedaiwa kuwa kundi lililobaki liliingia katika ofisi hizo hilo na kuweka vilipuzi vilivyotengenezwa kienyeji, ambavyo vililipuka muda mfupi baada ya watu hao kuondoka eneo hilo na kusababisha uharibifu wa wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.

Jeshi hilo limesema kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu waliofanya tukio hilo na kujua dhamira yao ili wafikishwe katika vyombo vya sheria kwani wajibu wa jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao na kamwe haliwezi kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchi

Aidha, jeshi hilo limewaomba waathirika wa tukio hilo na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio hilo

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles