» » Bulaya Aruhusiwa Kutoka Muhimbili

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja.

Bulaya alikimbizwa Muhimbili kutoka tarime mkoani Mara baada ya kupata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini Tarime. Alikuwa amelazwa wodi namba 18 katika jengo la Sewahaji akipatiwa matibabu.

Mbunge huyo wa Chadema, leo Agosti 28 ameruhusiwa kutoka hospitali na amewashukuru madaktari wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu ya kina.

Amesema afya yake imetengemaa lakini amepewa maelekezo kadhaa.

“Kwanza nitapumzika kwa siku 10, hivyo ndivyo nilivyoagizwa na nitatakiwa kurudi tena hospitalini kwa ajili ya kuangaliwa afya yangu zaidi. Kwa sasa nitapumzika kabla ya kurudi jimboni kuendelea  na shughuli za maendeleo,” amesema Bulaya.

Bulaya aliwekwa rumande Agosti 18 baada ya kukamatwa na polisi akidaiwa kuingia jimbo la Tarime kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi kwa mwaliko wa mbunge mwenzake Esther Matiko.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles