» » Mtu mmoja Afariki Kanisani Baada ya Kutoa Sadaka

Mkazi  wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) amekufa muda mfupi baada ya kutoa sadaka katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kilichopo katika Mtaa wa Makanyagio B.

Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa kigango hicho, Charles Kanyanda alisema Kangu ambaye ni mwanakwaya, alikuwa muumini wa Kanisa Katoliki, na Jumapili alihudhuria ibada ya Misa Takatifu kwenye kigango hicho ambayo ilifanyika saa moja na nusu asubuhi.

Alisema Beatrice alihudhuria ibada ya misa hiyo ambapo kwa kuwa alikuwa mwanakwaya aliingia kwenye nyumba ya ibada na kujiunga na wanakwaya wenzake iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu wa Dini (Katekista) wa Kigango, Agustino Ntalwila.

“Ibada ya Misa Takatifu iliendelea kama kawaida na ndipo ilipofikia muda wa kutoa sadaka na Beatrice alikwenda kutoa sadaka kama kawaida kisha akarudi kwenye nafasi yake na kuendelea kuimba ghafla baadaye alianguka na kupoteza fahamu.

Taharuki iliibuka kwenye nyumba hiyo ya ibada ndipo ilipobainika kuwa alikuwa amekata roho,” alieleza Kanyanda na kuongeza kuwa wanakwaya wenzake walijitahidi kumpatia huduma ya kwanza bila ya mafanikio.

Kanyanda alisema maziko yake yalifanyika katika makaburi ya Mwanga jana ambayo yaliongozwa na Paroko wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Maria Imakulata, Monsinyori, Padri George Kisapa aliyemwelezea alikuwa mcha Mungu na ameacha pigo kubwa kwenye kwaya ya Kigango cha Makanyagio B.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...