» » Jopo la kuchunguza tuhuma za Urusi labuniwa Marekani

Robert Mueller kulia ambaye aliwahi kuhudumu kama mkurugenzi wa FBI ndio anayesimamia jopo hilo

Image captionRobert Mueller kulia ambaye aliwahi kuhudumu kama mkurugenzi wa FBI ndio anayesimamia jopo hilo
Baraza maalum linalochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana linaarifiwa kuunda jopo kuu.
Gazeti la The Wall Street Journal linasema jopo hilo kuu la Robert Mueller limeanza kazi katika wiki za hivi karibuni na limewasilisha agizo la kukusanya ushahidi kuhusu mkutano wa Juni mwaka jana kati ya mwanawe rais Trump na wakili mmoja wa Urusi.
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa uchunguzi wa Robert Mueller'umechukua hatua ya kwanza kuelekea ufunguzi wa mashtaka ya uhalifu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters , jopo hilo la mahakama limewaita mashahidi kuzungumzia juu ya mkutano wa mwezi Juni mwaka 2016 baina ya mtoto wa kiume wa rais Donald Trump .. Trump Jr na wakili wa Urusi.
Rais Trump anapinga madai yoyote kwamba maafisa wake walikula njama na serikali ya Urusi ili kumshinda Bi Hillary Clinton katika uchaguzi wa urais.
Rais Putin na rais Trump
Image captionRais Putin na rais Trump
Nchini Marekani , jopo kubwa la mahakama huundwa kwa ajili ya kuchunguza ikiwa ushahidi uliopo ni wa kutosha kiasi cha kufungua kesi ya mashtaka ya uhalifu.
Jopo kubwa la mahakama hata hivyo haliamui juu ya kutokuwepo na hatia wala uwezekano mtu kuwa na hatia.
Taarifa ya kwamba jopo kubwa la mahakama limekuwa likikutana mjini Washington DC, na kwamba linachunguza mkutano wa June 2016 baina ya Donald Trump Jr na raia wa Urusi, ni wazi kwamba uchunguzi sasa unaelekezwa kwa wandani wa rais.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440





tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...