» » Jengo la Klabu ya Yanga Kupigwa Mnada Jumamosi Hii

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwapa pole watani wake wa jadi klabu ya Yanga kufuatia taarifa iliyotoka katika moja ya gazeti kuonyesha jengo lao litapigwa mnada Jumamosi ya wiki hii. 

 

Haji Manara ametoa pole hiyo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kuwaombea watani wao wajadi kwa kusema hivi sasa hali yao si nzuri hivyo kama jengo hilo litauzwa watakwenda kukaa wapi.

"Mungu wangu,Jumamosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit" alimalizia Haji Manara

Mbali na hilo klabu ya Simba na Yanga zote zipo visiwani Zanzibar zikijipanga kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii unaowakutanisha watani hao katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano ya tarehe 23 Agosti 2017. 


Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles