» » Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni


Wakili wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru.

Amedai hali hiyo inahatarisha afya ya mteja wake kwani akikosa kupata matibabu sahihi anaweza kupoteza maisha kutokana upasuaji aliofanyiwa uliosababisha kuwekewa maputo tumboni.

“Mara mbili mahakama ilitoa amri ikielekeza utawala wa Magereza kumpeleka mshtakiwa wa kwanza Muhimbili , amri ilitolewa baada ya mahakama kukubaliana na hoja za upande wa utetezi, lakini badala ya kumpeleka Muhimbili, Magereza walimpeleka mshtakiwa Hospitali ya Amana.

“Kwa taarifa za kitabibu ni kwamba hali ya mshtakiwa wa kwanza isipohudumiwa ipaswavyo inaweza kusababisha kifo kwani maputo yanaweza kupasuka tumboni , mahakama iliekeza mshtakiwa apelekwe moja kwa moja Muhimbili ambayo ni hospitali ya juu kabisa ya Serikali, ndio nategemea inaweza kuwa na wataalamu na vifaa thabiti kwa ajili ya matatizo yanayomkabili mshtakiwa wa kwanza,” amedai.

Makandege alidai amri zote zilizotolewa na mahakama hazijatekelezwa , aliomba mahakama itoe amri nyingine ya kuutaka upande wa Jamhuri kuamuru amri iliyotolewa itekelezwe.

Akijibu Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amedai Jamhuri haijakaidi amri ya mahakama na kwamba Magereza wana utaratibu wao ambapo wanahojiana na mgonjwa wakiona tatizo lake hawana utaalamu nalo wanampa rufaa kwenda Muhimbili. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo mshtakiwa Seth na James Rugemarila, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwa na mashitaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha hivyo kuwafanya wakose dhamana.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...