» » wanaume Waliooa wake wengi kufungwa jela Canada


 

Haki miliki ya pichaJEFF MCINTOSH/THE CANADIAN PRESSImage captionWinston Blackmore afika mahakamani huko Cranbrook

Viongozi wawili wa dini nchini Canada wamepatikana na hatia ya kuoa wake wengi.

Mahakama iliambiwa kuwa Winston Blackmore mwenye umri wa miak 61 alioa wanawake 24 naye mwanamume ambaye alikuwa ni mkwe wake James Oler akaoa wanawake 5.

Wote walipatikana na hatia ya shtaka moja la kuwaoa wanawake wengi na kila mmoja anakabiliawa na kifungo cha miaka mitano jela.

Wanaume maskini kuzuiwa kuoa wake wengi Nigeria

Hukumu hiyo imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kdini nchini Canada.

Blackmore na Oler ni kutokna jamii moja ya dini ya karibu watu 1500 ambayo ilianzishwa mwaka 1946.

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionJames Oler akifika kotini

Wote hao walikuwa ni makasisi wa dhehebu lililojitenga kutoka kanisa la Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS)

Bwana Blackmore alifukuzwa kutoka FLDS mwaka 2002 na mahala pake pakachukuliwa na bwana Oler.

Waliokamatwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa waachiliwa

Matawi ya dhehebu hilo yako nchini Marekani ambapo kuna wanachama karibu 10,000

Kuoa wanawake wengi ni haramu chini ya sheria za Canada, Palisi nchini Canada walianza kuchunguza dhehebuhilo mnamo miaka ya 1990.

Haki miliki ya pichaJONATHAN HAYWARD/THE CANADIAN PRESSImage captionWinston Blackmore mwaka 2008, inakisiwa ana watoto 145

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...