» » Trump: Tumechoka kuivumilia Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.

Image captionRais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.
Rais wa Marekani Donald Trump anasema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.
Katika hotuba ya pamoja na rais wa Korea Kusini Moon Jae, kwenye ikulu ya White house, Trump amesema kwamba vitisho vya Korea Kaskazini vinafaa kupata majibu ya kijasiri.
Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.
Rais wa Korea Kusini amesema kwamba taifa lake litaweka marekebisho ya kiuslama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.
Rais Moon pia amesema ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.
Kwengineko, Bwana Moon alisema kuwa ni muhimu kuendelea kujadiliana na viongozi wa Korea Kaskazini.
Bwana Moon alisema kuwa swala la Korea Kaskazini linafaa kupewa kipaumbele wakati wa mazungumzo akisisitiza kuwa ni usalama thabiti pekee unaoweza kuleta amani katika eneo zima la Pacific.
Akizungumza katika Ikulu ya Whitehouse, bwana Trump alisema kuwa wakati wa kuvumiliana na utawala Korea Kaskazini umefeli miaka mingi akiongezea: Kwa kweli uvumilivu huo umekwisha.
Kiongozi huyo wa Marekani amesema kuwa serikali yake sasa inafanya kazi na Korea Kusini pamoja na Japan wakiwemo washirika wengine duniani kuchukua hatua kadhaa za kidiplomasia, usalama na kiuchumi ili kuwalinda washirika wake pamoja na raia wa Marekani dhidi ya janga hilo kwa jina Korea Kaskazini.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...