Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa pili wa siri ambao haukutajwa ulipofanyika katika kikao cha mkutano wa mataifa ya G20, imebainika.
Walifanya mazungumzo baada ya mkutano wao wa kwanza lakini ukulu ya White House haijatoa maelezo kuhusu kile kilichozungumziwa.
Rais Trump amekana madai ya kufanyika kwa mkutano huo wa siri na Putin na kusema ni ''habari bandia''.
- Trump: Putin anamshinda Obama kwa uongozi
- Trump na Putin wawasiliana kwa simu
- Trump na Putin wakutana ana kwa ana
Uhusiano wa viongozi hao wawili unachunguzwa kufuatia madai kwamba kampeni ya Trump ilishirikiana na Urusi.
Wapelelezi wa Urusi wanaamini kwamba Urusi ilimsaidia bwana Trump kushinda uchaguzi wa mwaka jana kitu ambacho Urusi imekana.
Bwana Trump amepinga madai kama hayo.
Mkutano wa pili ulifanyika wakati wa chakula cha jioni cha viongozi katika kikao hicho cha G20 mjini Hamburg mapema mwezi huu
Rais wa Marekani alikuwa pekee na Putin alikuwa na mkalimani wake huku vyombo vya habari vya Marekani vikisema kuwa mkutano huo ulichukua saa moja.
- Donald Trump na Vladmir Putin kukutana ana kwa ana G20
- Trump: Ninaelewana vyema na Vladimir Putin
- Trump Junior alikutana na wakili wa Urusi
Madai ya kilichozungumzwa yaliwasilishwa kwa maafisa wa Ikulu ya Whitehouse na bwana Trump mwenyewe kwa kuwa hakukuwa na wasaidizi wakati wa mkutano huo.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI