SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 40.
Tulipoishia, Nikarudi nyumbani na kufanya usafi kisha nikaanza nikasikia jinsi ya kumpata baba yangu. Mara nikasikiwa kwenye tv ya mle ndani. "BREAKING NEWS" pembeni kulikuwa na picha yangu kisha nikasikia_______Songa sasa..... Mtu mmoja kwa jina Yusuph Ng'ahala maarufu kama afande Yuu anatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma mbalimbali. Popote umwonapo toa taarifa kituo cha polisi kilicho jirani na wewe. Maaskari wa jeshi la polisi wamepata ajali mbaya eneo la daraja la sarenda na wamepoteza maisha na kutokana nabajali hiyo mbaya hata sura zao hazitambuliwi. Ndugu yeyote mwenye mfanyakazi katika kituo hicho cha polisibafike mara moja bila kukosa. Nilifurahi kwa kuwa nilichokipanga kimeemda kama nilivopanga.
Swala la mimi kutangazwa na vyombo vya habari halikunitisha hata kidogo. Nikaamua moja tuu kumfuatilia baba yangu. Kwani mwanzo nilipewa taarifa kafa sasa huyu aliyekamatwa ni baba yangu halali si yule aliyezikwa haya yote nilikuwa nikiyahisi tangu mwanzo. Mazingira ya kifo cha baba yangu nikikuwa siyaelewi tangu mwanzo. Lakini kutokana na mimi kuzongwa na kuandamwa na akina Zabroni kulinifanya nisifuatilie kwa makini ila nilihisi huenda baba yangu hakufa ilikuwa mbinu za kunitega na kunidhoofisha. Basi nikatoka na kuamua kwanza niende kijijini ili niongee na mama nijue baba kapatikana vipi.
Hii ingenisaidia kujua wapi nianzie. Basi kuna sura moja ya bandia niliwahi kuikusanya katika upelelezi wangu kipindi nikiwa afande. Nikaona sasa huu ndio wakati muafaka wa kuitumia. Nilijiandaa na kwenda uwanja wa ndege ili nifike mbeya halaf niwahi kijijini. Safari yangu ilikuwa vizuri bila kushtukiwa. Baada ya kufika kijijini nilimkuta mama na kuanza kumwuliza jinsi baba alivyorudi. Ndipo akanambia kwanza inawezekana mtu tuliyemzika hakuwa baba yako kwani aliyekuja leo ndio yeye. Alidai kuwa walimfungia mahali na kumtesa sasa akafanikiwa kutoroka.
Lakini baada ya kufika tuu nyumbani na kujieleza akakamatwa kwa mara ya pili. Nikamwuliza mama hao watu walikuwaje? Mama akajibu mwanangu sijamwona hata mmoja. Nikaona hapana huenda huu pia ni mtego nikaingia kichwa kichwa mwisho ninase ngoja njia ni moja tuu kufukua kaburi la baba na kuchukua mifupa kisha nikapime DNA. Nikatafuta vijana sita hivi wenye nguvu kisha tukaenda kufukua na nikalikuta jeneza na kilifumua. Nikachukua mifupa kadhaa kisha tukafunga na kulirudisha na sisi tukarudi nyumbani. Niliwalipa wale vijana pesa yao kisha wakaondoka.
Niliongea na mama mbo mengi sana kwani nilihitaji kuondoka mda uleule. Vipimo vya DNA kwa kipindi hicho vilikuwa vinapatikana Dar hospitali ya muhimbili tuu. Nikaagana maye na kumuahidi ikiwa yule ni kweli ni baba yangu atarudi japo wengi wanajua kafa. Nikatoka na kuwahi uwanjani mara moja. Nilifika moda ya saa kumi na mbili jioni nikapata ndege inatoka saa moja usiku. Ilinibidi kuka kusubiri. Mifupa yangu sikuacha nilikuwa naho. Nimeitunza. Kuna mtu pale uwanjani alikuwa akiniangalia sana.
Sikujua mara moja ni anaangalia nini kwangu. Baada ya kuona vile nikaamua kuingia ndani ya chumba fulani ili nisubiri ndege kuondoka. Baada ya hapo kama kawaida ndege ikaanza Safari kurudi Dar es salaam. Nilifika Dar es salaamu na kuamua kuishi hotelini ili kuepuka usumbufu na watu. Nilipanga siku ya pili mchana niende muhimbili nikapime kama aliyezikwa ni baba yangu au laa!
Mda ulisonga kwa kasi sana nililala na asubuhi kulipokucha nadhani ilikuwa mida ya saa 12 asubuhi. Nilisikia mlango wangu unagongwa kule hotelini. Hapo nikainuka na kuandaa pete yangu ya kuulia. Nikainuka na kwenda kuufungua mara wakaingia polisi wawili kwa kasi sana kisha mmoja akasema uko chini ya ulinzi. Unafanya biashara ya kuuza viungo vya binadamu.
Nilishtuka san a nikawa najiuliza wamejuaje kuwa niko hotelini. Basi wakaanza kusachi bila utaratibu huku mimi nikiwatolea macho walipekua vitu vingi bila mafanikio basi wakaja kunihoji kwa nguvu. Mmoja akanipiga kofi na kuniuliza umeficha wapi viungo vya watu wenye ulemavu wa Ngozi.
Nilishangaa kwani mimi sijawahi kufanya huo uninga nikawa nawashangaa tuu. Mara wakaambiana waondoke wakaanza kutoka lakini kabla hawajaisha kuna mmoja akasema kuna kitu nilikiona hebu njoo tuangalie wakarudi ndipo nikamwona moja kwa moja anaenda nilipokuwa nimeweka ile mifupa miwili ya marehemu baba.
Hapo ilikuwa kosa la jinai nikamfuata na kumgusa begani. Mara akaaniangalia taratibu akawa anapoteza nguvu yule mwingine kuona vile naye akasogea asilolijua ni kuwa anajipeleka kwenye umauti. Alipokaribia tuuu sikulaza dau nilimtia kitu kichwani afe haraka. Kisha mi nikachukua funguo nikafunga mlango. Nikawa natafakari jins ya kutoka.
Wazo likanijia nitoweke pale na kutafuta sehemu nyingine. Nikaona niwahi mugimbili tuu nikaone vipimo vinasemaje ikiw vifaonyesha siho baba yangu basi kifuatacho Mungu anajua! Na ikiwa vitaonyesha ni baba yangu imekula kwao kwani sitaingia kwenye mitego yao ya kijinga tena. Nilifika muhimbili nikamkuta daktari mmoja ivi nikamwambia shida yangu akanambia nimpe ile mifupa nikampa akanambia njoo uchukue majibu kesho. Nilitoka na kurudi kujificha mpaka siku ya pili ndipo nikarudi kuchukua majibu. Nilimkuta daktari yule ambapo akaniuliza maswali kadhaa kisha akanikabidhi majibu ambayo yalionyesha kuwa_________________________________________
________________________________________________________________________________________________________________________,_Cheki na mimi sehemu ya 41 tujue majibu ya baba. Nawapenda wote jamani kwa lolote nichek kwa namba na mawasiliano ayo ya juu. Chaooooooooo
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 40.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment