MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 39.
Tulipoishia, Mi sikua najali hayo mimi nilikuwa najali kama napata pesa tuu basi. Kuna siku nikiwa uwanja wa ndege wa mwl Nyerere Kuna askari wawili walikuwa wakiniangalia sana. Nikiwa nataka kuwakwepa nikaona wanasogea karibu yangu. Wakafika kisha______Songa nayo........ Mmoja akaniuliza habari yako kijana? Nikajibu kwa kujiamini nzuri tuu poleni na kazi! Wakajibu ahsante kisha wakaendelea samahani, nikawajibu bila samahani. Wakaanza sisi ni maafisa polisi tunalinda usalama wa taifa. Tumekuona hapa tukaona si vibaya tukihitaji maelezo yako ofisini kwetu. Vipi kwani kuna chochote kibaya mnanihisi? Hapana ni kwasababu za kiusalama tuu tunakuomba. Nikajibu sawa.
Tukaondoka kuelekea ofisini kwao na nilipofika tuu. Wakaanza kijana tuna taarifa zako nyingi hapa ofisini kwetu. Moja kubwa ni kuwa wewe ni mtuhumiwa wa ujambazi. Pili unauza madawa ya kulevya, zaidi unafanya biashara ya kuuza binadamu ambapo unawapata kwa udanganyifu, Halafu pia kuna tuhuma nyingine nyingi zikikuhusisha na mtandao wa kihalifu huu hapa. Akanipa orodha ya picha ambapo juu kabisa nilimwona Zabroni na chini zilifuata picha za Peris na wengine wengi ambao mimi niliwahi kuwafuatilia. Akaniuliza je wewe si ndie huyo wa kwanza? Nikatabasamu kidogo kisha nikajibu Afande nasikitika sana kwa kuwa umenihusisha na tuhuma zisizo na ukweli. Mimi ni askari kama wewe na pia nafuatilia kesi hii hii na pia si mara ya kwanza kukamatwa ninachoweza kusema ni kuwa labda nikupe kitambulisho changu cha kazi. Nikaingiza mkono ndani ya koti na kutoa bastora kisha kwa haraka nikawafyatulia risasi wale maaskari wawili. Ilikuwa imefungwa kifaa cha kuzuia kelele hivyo wakati nawaua hakuna aliyesikia.
Nikatoka nje na kupotea. Nilifika kwa yule dada nikiwa nimeghafirika sana kwani nilianza kuona mwisho wangu utakuwa aibu ikiwa nimeanza kuhisiwa nikaona njia ni moja tuu. Kuua. Nikamfuata ambapo akasema haa Yuu umekuja vipi za utokako? Nikamwangalia jicho fulani kisha nikamjibu za nitokako ni hizi. Nilikuwa na pete kiganjani yenye mwiba wa sumu nikamdunga nayo. Kisha akashtuka na kuniangalia. Baada ya sekunde kadhaa alianguka chini na kupoteza maisha. Chaajabu wakati natoka mle nikamwona mwanaharamu mmoja akiingia mle si mwingine alikuwa ni yule wa jela aliyenitorosha hapo ndipo niliona hasira ikikuwa na kunivamia kisha nikaanza kumfuata. Aliponiona akaanza kukimbia. Nilimwangalia kwa makini uchochoro alioingia nikakatisha nikawahi mbele. Ile anatokeza hivi akakutana na ngumi ya haja akaanguka chini. Sikutaka maelezo yoyote zaidi ya kuua. Hayo tuu ndo yalikuwa maelezo sahihi kwangu kwa kipindi hiki.
Nikatoa pete yangu na kumchoma nayo.kisha nikamwacha akigalagala pale mi nikatokomea zangu. Nikiwa njiani nilipigiwa simu mara baada ya kuangalia alikuwa ni mama kijijini ambapo alisema kuna uvamizi umetokea nyumbani baba yangu kachukuliwa na watu wasiojulikana. Niliingiwa na hasira na uchungu nikajihisi mbona mimi kila ninachofanya hakuna jema! Nimesaidia nchi yangu nikalipwa mabaya, nimesaidia wakuu wangu wa kazi nikalipwa jela. Nimeanza kuuza madawa serikali ileile inanisumbua nifanye nini chema hapa duniani? Nini wanadamu mnataka nifanye? Ni nini mahitaji yenu kwangu? Kwani nimekosea nini duniani? Sasa langu moja tuu. Sijali muhuri wa nani wala wa nani. Sitaki tena madawa, sitaki kuuza watu ninachotaka ni uhuru wa maisha yangu. Nitautafuta popote kwa njia yoyote ile.
Nikaamua kuelekea nyumbani kwangu na kupumzika kiasi. Nilipofika nyumbani nikampigia simu mamayangu nikamwambia mama usiwe na shaka baba atapatikana tuu kuwa na amani tuu. Mama aliitikia kwa unyonge sana lakini hakua na jinsi. Nililala asubuhi kama saa kumi na mbili hivi nilisikia mlio wa gari aina ya land cruiser kwakua nilikuwa na uzoefu nazo nilijua tuu ni ya polisi hapo ndipo nikasema liwalo na liwe hakamatwi mtu. Mpaka nihakikishe nimelipa kisasi hapo ndipo nitajisalimisha mikononi mwa polisi. Nikaanuka na kujiweka sawa kisha nikaandaa silaha zangu nikakaa tayari. Mara nikasikia mlango wangu unagongwa. Sikutaka kufungua nilichokifanya nikatoa komeo na kuacha kawaida. Basi mmoja akasikika akisema tuuvunjeni kwani taarifa za uhakika zinasema yupo humu ndani.
Basi wakajikusanya na kuusukuma kwapamoja kwa nguvu. Kwakuwa mlango ulikuwa wazi iliwafanya wote kuanguka chini na kunipa kazi nyepesi ya kumimina risasi bila kuchoka. Baada ya sekunde 15 hivi mle ndani mligeuka bwawa la damu. Hakuna hata askari mmoja alikuwa akihema. Walikuwa kama wanne hivi. Kizuri ni kwamba wote wale niliwahi kuwakuta kwenye mtandao wa Zabroni hivyo nilikuwa nimepunguza vikwazo kwa kazi yangu. Mbele yangu nilikuwa nakabiliwa na mtihani mmoja mkubwa kumwokoa baba yangu nisiyejua yuko wapi na pia kulipa kisasi.
Baada ya pale nikabeba zile maiti na kupakia kwenye gari kisha nikaliwasha gari na kuelekea nalo sehemu fulani hivi. Niliendesha gari mpaka eneo lile nililolitaka kisha nikafika na kusimama. Nikawapanga vizuri na kuliweka gari katika gia kisha nikatafuta jiwe kubwa na zito. Nililiingiza kwenye gari na kuliweka sehemu ya ambayo hufanya gari liondoke. (Madereva wamenielewa) kisha nikaliachia.
Taratibu gari likaanza kusogea na kuongeza mwendo. Kwakua lile eneo lilikuwa na mteremko mkali gari ilienda kwa kasi sana. Na hapakuwa na mtu wa kuliongoza taratibu likawa linaacha njia na kuelekea mtoni. Lilienda kwa kasi sana na hatimaye likatumbukia mtoni vibaya huku likitanguliza sehemu ya mbele. Lilifika chini na kujikunja kiasi cha kwamba halikufaa tena kutumika. Hivyo ndivyo ilikuwa malengo yangu. Nikarudi nyumbani na kufanya usafi kisha nikaanza nikasikia jinsi ya kumpata baba yangu. Mara nikasikiwa kwenye tv ya mle ndani. "BREAKING NEWS" pembeni kulikuwa na picha yangu kisha nikasikia_____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Tukutane sehemu ya 40 tujue yaliyojiri huko! Nikutakie kazi njema na ujenzi mwema wa taifa letu.
SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU? SEHEMU YA 39.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment