» » Rais Magufuli: Siku Hizi Wazee Wako Shapu Kuliko Vijanya

Rais Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi, na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi, na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30.

Rais John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani hao ndiyo viongozi wa kesho.

Rais amezungumza hayo jana  wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini Tabora, ambapo aliweka wazi kwamba wanaowapa mimba watoto wa shule siyo  vijana pekee bali wapo wazee nao wameingia kwenye mkumbo huo hali ambayo inawafanya mabinti washindwe klumaliza elimu ya sekondari.

“Wazee siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao. 

".....Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.

Pamoja na hayo Mhe. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa kitanzania elimu.

"Tumeamua kutoa elimu ndiyo maana tumetenga bilioni 18.777 tunataka watoto wasome na wasipate mimba, naomba wajiepushe na mimba mpaka watakapotimiza malengo yao," aliongeza.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...