» » Rais Magufuli: Nitachomoa mwingine mwenye akili kutoka upinzani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefunguka na kuahidi kuwa bado ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo

Ameyasema hayo jana  alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, ambapo alisema kuwa maendeleo ya nchi hayana vyama ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.

“Maendeleo hayana chama ndiyo maana unaona nimeweza kuteuwa baadhi ya viongozi kutoka tena kwenye chama kidogo, na nitaendelea kuchomoa watu wenye akili akili kutoka kwenye vyama mbalimbali nitawaacha vilaza huko huko,”alisema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, kwa upande wake, Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni mwanachama wa ACT- Wazalendo ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wananchi na kutambulishwa alifunguka na kusema kuwa, Rais Magufuli amevunja mwiko wa Serikali kuwa ikiongozwa na watu kutoka chama kimoja baada ya kumteua yeye kuwa Katibu Mkuu wa Maji pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...