» » Halima Mdee aachiwa kwa dhamana ya Sh10 milioni


Mbunge. wa Kawe, Halima Mdee ameachiwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa siku sita.

Mdee ameachiwa leo Julai 10, kwa dhamana ya Sh10 milioni na wadhamini wawili, baada ya kusomewa shitaka la kutumia lugha chafu na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Mbunge huyo, alikamatwa Julai 4 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliyeamuru awekwe mahabusu kwa saa 48.

Hapi alidai, Mdee amemkashifu Rais na ndicho chanzo cha kutupwa rumande kwa saa hizo.

Wakili Katuga amedai kwamba, mnamo July 3, mwaka huu katika Ofisi za CHADEMA makao makuu, alimtukana Rais Magufuli kwa kumwambia anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afunge break.

Baaada ya kusomewa shtaka hilo Halima Mdee alikana kosa hilo na kesi imehairishwa kutokana na upelelezi kutokamilika mpaka tarehe 7 mwezi wa 8 mwaka huu ambapo kesi itatajwa tena.



Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...