» » Waziri Mkuu: Marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya nchi bila kibali na kuwataka wafanyabiashara kuuza chakula kwenye maeneo yenye uhaba nchini.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana, Jumatatu wakati akihutubia Baraza la Eid katika Msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu huyo alisema kuwa kuna maeneo ambayo wananchi hawakupata chakula vizuri kutokana na uhaba wa mvua hivyo wafanyabiashara wapeleke chakula kwenye maeneo hayo.

“Serikali bado haijatoa kibali cha kutoa chakula nje ya nchi, kama unaona kuna umuhimu kaombe kibali, lakini utapewa kibali cha kusaga upeleke unga na siyo mahindi,”amesisitiza  Majaliwa.

Majaliwa ameonya kuwa kwa wale watakao kamatwa wakisafirisha mahindi nje ya nchi kinyume na utaratibu, mahindi hayo yatataifishwa na kupelekwa kwenye ghala la Taifa na magari yatapelekwa polisi.

Amesema kuwa Serikali imepokea barua za maombi ya kupeleka chakula nchi jirani, lakini bado haijatoa ruhusa.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...