» » Watu wenye silaha washambulia eneo la watalii Mali

Le Campement Kangaba, eneo lililoshambuliwa

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionLe Campement Kangaba, eneo lililoshambuliwa
Vyombo vya Usalama nchini Mali vinasema vimeokoa zaidi ya wageni thelathini kutoka katika kituo kimoja cha Utalii, kilichokuwa kikishambuliwa na watu waliokuwa na silaha.
Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Salif Traore amethibitisha kuuawa kwa watu wawili, baada ya watu wanaohisiwa kuwa ni wapiganaji wenye itikadi kali kushambulia eneo hilo la starehe la Le Campement Kangaba lililoko nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.
Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Usalama, mmoja wa washambuliaji hao alifanikiwa kutoroka, baada ya kujeruhiwa, huku akiacha bunduki na chupa zilizokuwa na vifaa vya milipuko.
Aidha amesema watu wawili akiwemo raia mmoja pia walijeruhiwa.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yalifika katika eneo la tukio.
Wanajeshi wa Ufaransa eneo la tukioHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanajeshi wa Ufaransa eneo la tukio
Kituo hicho cha utalii ni maarufu nyakati za juma la wiki na kuwa kivutio kwa raia wa Mali wenye uwezo na wale wa kigeni wanaoishi Bamako.
Mapema mwezi huu, Ubalozi wa Marekani mjini Bamako ulionya uwezekano wa kutokea mashambulizi katika siku za baadaye katika majengo ya wanadiplomasia wa magharibi na maeneo mengine katika mji wa Bamako ambako raia wa nchi za magharibi wanapenda kwenda.
Wapiganaji wa Kiislamu wameendelea kufanya mashambulizi nchini Mali licha ya kupoteza maeneo yao wanayoyashikilia wakati wa uvamizi uliofanywa na majeshi ya muungano yaliyokuwa yakiongozwa na Ufaransa mwaka 2003.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...