» » Wasichana waliojifanya Waislamu wakamatwa Nigeria

Vazi la Hijab ni haki kwa wasichana wa Kiislamu kulivaa

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionVazi la Hijab ni haki kwa wasichana wa Kiislamu kulivaa
Wasichana saba waliojifanya kuwa Waislamu kwa kuvaa vazi la hijab wamekamatwa nchini Nigeria kwa kujaribu kufanya safari haramu ya barani Ulaya ,kulingana na maafisa.
Wasichana hao ni miongoni mwa watu 12 waliokamatwa na maafisa wa uhamiaji mapema wiki hii walipojaribu kuvuka mpaka kaskazini mwa jimbo la Katsina wakielekea Ulaya.
Mamlaka ya uhamiaji inasema kuwa wasichana hao saba wanatoka Kusini mwa taifa la Nigeria, na walivalia vazi la Kiislamu ili kuwasaidia kupita kwa urahisi katika mpaka katika eneo la kaskazini lililo na Waislamu wengi.
Baadhi ya waliokamatwa walinukuliwa wakisema kwamba walitaka kwenda Ulaya ili kutafuta ajira kutokana na hali ngumu ya maisha nchini Nigeria.
Wasichana hao baadaye walikabidhiwa kwa kitengo cha kukabiliana ulanguzi wa watu kwa uchunguzi zaidi.
Takriban watu 40 wamekamatwa katika kipindi cha miezi minne iliopita nchini Nigeria wakijaribu kuvuka na kuingia nchini Niger ili kuelekea Libya kupitia jangwa la sahara kabla ya kuabiri boti na kuelekea Ulaya.
Wakati huohuo zaidi ya watu 1000 waliripotiwa kurudi wenyewe nchini Nigeria kutoka Libya katika kipindi cha miezi mitano.



Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles